January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ronaldo awatolea uvivu waandaji tuzo Ballon d’Or

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo amemjia juu muandaaji wa tuzo ya Ballor d’Or Pascar Ferre ambaye pia ni mhariri wa Gazeti France Football ambalo linamiliki tuzo hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kupitia ukurusa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram muda mchache kabla ya kutolewa tuzo hiyo siku ya jana tarehe 29, Novemba 2021, mchezaji huyo aliandika kuwa mhariri huyo amewadanganya watu mara baada ya kusema kuwa ameongea na Ronaldo kuhusu malengo yake.

Ronaldo aliabdika kuwa anashangaa kuona Pascar Ferre wiki iliyopita alisema kwamba alimueleza kuwa malengo yake kwenye soka ni kustaafu mchezo huo, huku akiwa na tuzo nyingi za Ballon d’Or kuliko Messi

“Leo naeleza kwa nini kauli ya Pascal Ferré wiki iliyopita alisema uongo, alisema nimemwambia ndoto yangu ni kumaliza soka nikiwa na tuzo nyingi za Ballon d’Or kuliko Lionel Messi, amedanganya na kutumia jina langu kwa ajili ya kujitangaza na ku-promote Magazine anayofanyia kazi”

“Hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki kwa Mtu ambaye anaandaa tuzo yenye heshima kama hii anadanganya kiasi hiki, hiyo ni kumvunjia heshima Mtu ambaye amekuwa akiheshimu France Football na Ballon d’Or siku zote” aliandika Ronaldo

Mshambuliaji huyo ambaye ni staa mkubwa duniani kwenye mchezo wa soka ni moja ya watu maarufu wenye wafuasi wengi kwenye mtandao huo wa kijamii wa Instagram.

Ronaldo kwa sasa anajumla ya wafuasi milioni 371, huku akishinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or mara tano akiwa nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi aliyetwaa tuzo hiyo mara saba.

Pascar Ferre, mhariri Mkuu wa Gazeti la France Football, waandaji wa tuzo za Ballon d’Or

Aidha Ronaldo aliendelea kuandika kuwa, Mhariri huyo aliendelea kuwadanganya watu tena siku ya jana, kuwa kukosekana kwake kwenye hafla ya tuzo hiyo ni kutokana na muasala ya karantine

“Ferre pia amedanganya tena leo akijaribu kuelezea kuwa kukosekana kwangu katika hafla ya tuzo leo ni kutokana na masuala ya karantini, nitampongeza yoyote atakayeshinda tuzo hiyo, huo ndio uanamichezo na uungwana michezoni ambao umenikuza kisoka”

“Siku zote nimekuwa nikishinda kwa ajili yangu na vilabu ninavyovitumikia, ndoto yangu kubwa ni kushinda mataji kwa ajili ya Nchi yangu na vilabu ninavyotumikia na ndoto yangu nyingine kubwa ni kuwa mfano mzuri kwa wale wote wenye ndoto za kuwa Wacheza soka professional“ alimalizia Ronaldo

Mara baada ya kaundika hayo siku ya jana muda mchache uliofuata, Lionel Messi alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya saba, huku akiwabwaga, Robert Lewandowsk kutoka Bayrn Munchen na Mohammed Sarah wa Liverpool.

 

error: Content is protected !!