September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Robo fainali Uefa, Europa hadharani

Spread the love

SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya (Uefa) limetoa ratiba ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya droo iliyochezeshwa leo mapema, anaandika Erasto Masalu.

Katika ratiba hiyo, Manchester City ya England watamenyana na PSG ya Ufaransa, mabingwa watetezi, Barcelona watamenyana na wapinzani wao wa la Liga, Atletico Madrid, wakati vigogo wengine wa Hispania, Real Madrid watamenyana na Wolfsburg ya Ujerumani.

Bayern Munich ya Ujerumani watamenyana na Benfica Ureno katika Robo Fainali ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu.

Barcelona imeifunga mara zote mbili Atletico Madrid katika La Liga msimu huu, 2-1 kila mechi na mchezo wao unatarajiwa kuwa Robo Fainali tamu zaidi ya zote za Ligi ya Mabingwa mwaka huu.

Mechi za Robo Fainali zinatarajiwa kuchezwa Aprili 5 na 6, wakati marudiano yatakuwa Aprili 12 na 13.

Katika hatua nyingine, Uefa pia imetangaza ratiba ya Ligi ya Ueropa ambapo Borrusia Dortmund itavaana na Liverpool, Sevilla itacheza na Athletic Bilbao, Braga itakupambana na Shakhtar wakati  Villarreal itakutana na Sparta Prague.

error: Content is protected !!