July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Robo fainali Kombe la Shirikisho Machi 26

Spread the love

ROBO Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya mwisho wa mwezi Machi mwaka huu, huku timu nane zikichuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, anaandika Regina Mkonde.

Machi 26, 2016 utachezwa mchezo mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakuwa wenyeji wa wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba.

Alhamisi ya Machi 31, 2016, Yanga watawakaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku Azam FC wakiwa wenyeji wa Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mchezo wa mwisho wa robo fainali utachezwa Aprili 6, 2016 kwa Simba kucheza dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Aprili 7, 2016 itachezeshwa droo ya hatua ya nusu fainali ya kombe hilo.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.

error: Content is protected !!