September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Robo Fainali FA Cup: Simba vs Azam FC, Yanga vs Kagera

Spread the love

BIGWA wa Mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba itaikalibisha Azam FC kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam, huku klabu ya Yanga itamenyana na Kagera Sugar katika hatua hiyo hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Droo hiyo ambayo imechezwa leo kwenye makao makuu ya Azam TV ikiongozwa na Baraka Kizuguto, Meneja wa Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kuonesha kuwa michezo hiyo itapigwa tarehe 26 na 27 Juni, 2020, huku hatua ya nusu fainali ikitarajia kuchezwa tarehe 12 Julai, 2020.

Azam FC ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo baada ya kumfunga Lipuli FC kutoka Iringa itakuwa na wakati mgumu mbele ya Simba baada ya kufungwa katika michezo yote miwili ya Ligi Kuu Bara katika msimu huu.

Kwa upande wa Yanga watakuwa na deni la kulipiza kisasi mbele ya Kagera Sugar baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwenye msimu huu licha ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao kwa siku za hivi karibuni.

Michezo mingine ambayo imepangwa kwenye droo hiyo ambayo klabu ya Sahare All Stars itavaana na Ndanda FC huku Namungo FC watakuwa nyumbani kuwakalibisha Allience FC kutoka Mwanza.

error: Content is protected !!