May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Robo fainali Euro kupigwa Ijumaa, Uingereza kuwavaa Ukraine

Spread the love

 

MIAMBA nane itachuana katika hatua ya robo fainali ya michuano ya
Euro 2020 kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 2 na 3 Julai 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya kuhitimishwa kwa hatua ya 16 bora, iliyoshuhudia miamba mingine ya soka ikitolewa.

Timu zilizosalia ambazo zitauamana hatua ya robo fainali ni Uswizi itacheza na Hispania saa 1:00 usiku, huku Ubelgiji ikiumana na Italia saa 4:00 usiku. Mechi hizo zitachezwa tarehe 2 Julai 2021.

Robo fainali nyingine, itachezwa tarehe 3 Julai 2021, ikihusisha Czech Republic dhidi ya Denmark saa 1:00 usiku huku Ukrain ikikwaana na Uingereza saa 4:00 usiku.

Baadhi ya mataifa yaliyotolewa hatua ya 16 bora ni mabingwa watetezi Ureno waliovuliwa ubingwa huo na Ubelgiji kwa kipigo cha 1-0.

Baada ya dakika 120 kumalizika katika ya Ufarasa na Uswizi zikiwa zimefungana 3-3, Uswizi ilisonga mbele kwa mikwaju ya penati 5-4. Ujerumani ilijikuta ikitupwa kando ya michuano hiyo na Uingereza kwa kipigo cha 2-0.

Fainali ya michuano hiyo, itapigwa Jumapili ya tarehe 11 Julai 2021.

error: Content is protected !!