Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa RITA yapitisha Bodi ya Wadhamini CUF Lipumba
Habari za Siasa

RITA yapitisha Bodi ya Wadhamini CUF Lipumba

Spread the love

KATIKATI ya mgogoro wa makundi mawili ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) imesajili majina manane kuunda Bodi ya Wadhamini ya chama hicho. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Taarifa ya uundwaji wa bodi hiyo iliyopitishwa na Rita imetolewa leo tarehe 8 Machi 2019 na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara anayetoka katika kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa CUF anayeungwa mkono na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Akiwa kwenye Ofisi Kuu  ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam Sakaya ambaye anatambuliwa na CUF Lipumba kama Kaimu Katibu Mkuu wa CUF amesema, bodi hiyo sasa ni halali baada ya kusajiliwa rasmi na Rita licha ya kuwepo kwa mvutano wa awali.

Hatua ya CUF Lipumba kupeleka majina na kusajiliwa Rita inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa siku 18 zilizopita wa kufuta bodi ya Lipumba iliyokuwa imesajiliwa Rita na pia kukataa majina yaliyopelekwa na Kambi ya Maalim Seif Shariff Hamad kwa madai zote hazikukidhi vigezo.

“Tuliwasilisha upya maombi kwenye ofisi ya RITA ili bodi yetu iweze kusajiliwa, kwa hiyo nafurahi kuwajulisha rasmi kwamba, nimetumiwa barua rasmi tarehe 6 mwezi huu kutoka Rita na sasa bodi yetu imesajiliwa rasmi,” amesema Sakaya.

Akizungumza na MwanahALISI ONLINE hivi karibuni, Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya CUF Kambi ya Prof. Lipumba alisema uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kufuta bodi ya awali ni wa kisheria na kuwa, kinachofuata kwa sasa ni kufuata utaratibu ili kuwa na bosi iliyokidhi vigezo.

“Athari yake ni kwamba, usipokua na bodi na hasa kwenye chama chenye kupata ruzuku ya serikali athari yake hamtaweza kupata ruzuku ya serikali.

“Ni kwa sababu sheria inahitaji bodi ya wadhamini ya chama kwa kuwa hao ndio wamiliki wa akaunti ya chama ambapo ruzuku ndio hupitishwa hapo,” amesema Kambaya.

Hata hivyo, hivi karibuni CUF Maalim nayo ilieleza kupeleka majina ya wajumbe ili kuunda Bodi ya Wadhamini ya chama hicho ambapo mpaka sasa haijaelezwa nini kinaendelea.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!