Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko RITA watakiwa kusaka kiini mwitikio mdogo kuandika wosia
Habari Mchanganyiko

RITA watakiwa kusaka kiini mwitikio mdogo kuandika wosia

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Wizara Katiba na Sheria, Mary Makondo amewataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kukusanya maoni kwa wananchi ili kutambua kiini kinachosababisha kuwepo mwitikio mdogo katika kuandika wosia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza mapema jana tarehe 19 Julai, 2022 jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa wizara hiyo na wadau mbalimbali katibu Mkuu huyo alisema RITA wanatakiwa kufanya hivyo ili kubaini sababu za mwitikio mdogo na kuzirekebisha sababu hizo ili kupunguza migogoro ya mirathi ambayo kwa kiasi kikubwa waathirika ni wanawake na watoto.

Mary aliwapongeza RITA kwa hamasa kubwa wanayoitoa lakin alisema licha ya hamasa hiyo bado watanzania wanaojitokeza ni wachache.

“Hamasa ipo inatolewa lakini watanzania bila kujali  umuhimu wa kuandika wosia wanajitokeza wachache,”

Aliwataka RITA kuandaa dodoso lipelekwe kwa wananchi na waeleze sababu zinazowafanya washindwe kuandika na kutunza wosia.

Naye Mtendaji Mkuu wa Rita, Angella Anatory alisema mamlaka hiyo imepokea wosia 700 pekee idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na takwimu za namba ya watanzania.

Alisema wanatambua kuwa kuna taasisi nyingine zinazohusika katika uandaaji na utunzaji wa wosia kama benki na wanasheria binafsi lakini upande wa Serikali, Rita ndio inafanya kazi hiuo niwasisitieze watanzania kuandika wosia.

Alisema wanapokea maelekezo ya wizara na kuyafanyia kazi na tayari wameandaa dodoso ya ndani kwanza ipitiwe na menejimenti kabla ya kuipeleka kwa wananchi tupate maoni yao kwanini wanakuwa wazito kuandika wosia.

Katika hatua nyingine Mary alieleza kuwa Serikali itaendeleza programu ya usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano baada ya kumalizika muda kwa programu inayowezeshwa na wahisani.

Alisema kwa sasa Rita inatekeleza programu hiyo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ambapo jumla ya watoto 7.7 milioni wamesajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!