March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

RITA kuwafuata wananchi mikoani

Emmy Hudson, Kaimu Msajili Mkuu wa Vizazi na Vifo

Spread the love

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeanza maboresho ya Mkakati wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu (CRVS) ambao utatatua changamoto  zinazosababisha wananchi wengi kushindwa kujisajili kutokana na sababu mbalimbali, anaandika Jovina Patrick.

Emmy Hudson, Kaimu Msajili Mkuu wa Vizazi na Vifo amesema kuwa mkakati wa usajili umeanza kutekelezwa  kwa kundi la watoto  wenye umri chini ya miaka mitano katika mikoa saba ambayo ni Mbeya, Mwanza, Iringa, Njombe, Geita, Songwe na Shinyanga.

“Mikoa hiyo watoto walio na umri chini ya miaka mitano watafanyiwa usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa vinavyojazwa kwa mkono bila kutozwa malipo yoyote katika ofisi za watendaji wa kata na vituo vya huduma ya afya.

“Cheti cha kuzaliwa kilichojazwa kwa mkono ni cheti halali kama ilivyo kwa vilivyochapishwa kwa mashine hivyo vinaweza kutumika mahali popote kupata huduma,” anasema Emmy.

Mtendaji huyo amezitaka taasisi zote nchini kuvikubali vyeti hivyo vinapowasilishwa ili kupata huduma mbalimbali  na endapo kutakuwa na mashaka yoyote zisisite kuwasiliana na ofisi za RITA na sio kuvikataa.

error: Content is protected !!