July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RITA kufuta taasisi 76

Kaimu Msimamizi Mkuu wa Wadhamini wa Rita, Emmy Hudson

Spread the love

WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imetoa siku 30 kwa taasisi ambazo hazijafanya mrejesho wa mwaka wa fedha na kukamilisha taarifa zake, vinginevyo zitafutwa. Anaadika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Msimamizi Mkuu wa Wadhamini RITA, Emmy Hudson ametaja jumla ya idadi ya taasisi hizo kuwa ni 76.

Kwa mujibu wa RITA, hadi sasa kuna jumla ya taasisi 5165 zilizosajiliwa ambazo ni pamoja na madhehebu ya kidini, vilabu nya michezo, vyama vya siasa na taasisi binafsi.

Wakati akitoa ufafanuzi Hudson amesema, wanatarajia kuzifuta taasisi hizo kutokana na muongozo wa sheria ya muunganisho wa wadhamini ya mwaka 2002, sura ya 318.

Amesema, taasisi hizo zitafutwa ndani ya muda huo endapo wahusika hawatatoa ufafanuzi na maelezo ya kutosha juu ya ukimya wao.

Taasisi hizo zimegawanyika katika makundi mawili, ambapo 49 zipo Dar es Salaam na 29 zinatoka nje ya mkoa wa huo na kwamba, kati ya hizo 29 ni za kidini na zilizobaki ni za kijamii.

“Zipo taasisi ambazo zimekuwa zikikaidi na kukiuka utaratibu. Mwisho mwa mwaka 2014 RITA kupitia vyomba vya habari ilichukua jukumu la kuwakumbusha wadhamini kufanya mrejesho kama inavyoagiza sasa watu kama hawa wasiofuta maelekezo inabidi wachukuliwe hatua,” amesema Hudson.

Aidha, ametoa wito kwa wadhamini wote ambao hawajakamilisha mjerejesho wao kutokana na sababu mbalimbali kufanya hivyo mapema kabla hatua kali kuchukuliwa.

“Bado tuaendelea na uchambuzi wa taasisi ambazo hazijakamilisha mrejesho pamoja na kuwasilisha mahesebu ya mwaka wakamilishe kabla ya hatua ya kuzifuta hazijachukuliwa.

“Hata kama jina la taasisi kwenye orodha ambazo zipo kwenye mtandao wetu halipo inabidi wadhamini watekeleze,” amesema.

error: Content is protected !!