January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RITA kuanzisha mfumo mpya wa kukusanya taarifa

Mtoto mchanga muda mcheche baada ya kuzaliwa

Spread the love

WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Tanzania (RITA), unatarajia kuanzisha mfumo wa mpya ya kukusanya taarifa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mfumo huo utachukua na kuhifadhi matukio muhimu kama vile ya vizazi, vifo, ndoa na talaka pamoja na sababu zake (Civil Registration and Vital Statistics- CRVS).

Mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa RITA na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Watoto Duniani (UNCEF) na Serikali ya Canada, unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam jana, Phillip Saliboko- Afisa Mtendaji na Msajili Mkuu wa RITA amesema “CRVS utaongeza kasi ya kufikia Malengo ya millennia yatakayopagwa baada ya mwaka huu”.

“Baada ya kukusanya taarifa na sababu zake. CRVS itasaidia kupambana na adui maradhi, ujinga, umasikini na kurahisisha utaratibu wa wananchi kupata haki zao za msingi, ikiwemo haki ya mtoto kupewa jina na kutambulika kisheria,” amesema Saliboko.

Aidha, Saliboko amesema, RITA itahakikisha inakuwa na mwakilishi katika kila hospitali, ofsi za kata, mitaa na vijiji ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.

Amesema, “watu waliozaliwa kuanzia mwaka 1985 ndio ndio tuna taarifa zao. Nchi ina changamoto katika suala la utambuzi. Sheria haikulazimisha wananchi kujisajili, hivyo CRVS itarahisisha utendaji wetu”.

“Ni lazima tuweke mfumo ambao utasaidia vizazi vijavyo. Kuna watu ambao wanazaliwa na kufa lakini hawajawahi kusajiliwa mahali popote,” ameongeza.

error: Content is protected !!