
Mwanasheria wa RITA, Joseph Mwakatobe akitoa maelezo kuhusu mirathi, kwa Jason Rwiza
WAAJIRI nchini wameshauriwa kuwasisitiza wafanyika wao, kujenga tabia ya kuandika wosia na kuachana na dhana kuwa kufanya hivyo ni kujichuria. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).
Aidha, imeelezwa pamoja na jitihada za taasisi mbalimbali kuhamasisha wananchi kuandika wosia bado mwamkoni mdogo kutokana na Imani kwamba kufanya hivyo nikujitabiria kifo wengi wakiita uchuro.
Hayo yalibainishwa Jijini Dar es Salaam na Meneja masoko wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita), Josephat Kimaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
“Kuacha kuandika wosia imepelekea kuongezeka kwa idadi ya mashauri ya Mirathi mahakamani yanayo chukua muda mrefu kumalizika tumeshuhudia familia nyingi zikidhulumiwa mali na ndugu wamarehemu kupelekea hata wengine kushindwa kumudu maisha ya mwananchi wa kawaida”amesema Kimaro.
Kimaro amesema Changamoto zilizotajwa zimekuwa pia zikizikumba familia zaWafanyakazi waliofariki kwa mfanyakazi nimuhimu sana kuandika wosia kwani ndani yake ataeleza hata nani atafatilia mafao na stahili zake mahali alipokuwa akifanya kazi na jinsi gani kinachopatikana kitumiwe.
Kimaro anasisitiza kuwa wosia mashauri ya kawaida inabidi kufunguliwa mahakamani na mara kadhaa imetokea kuteuliwa msimamizi wa mirathi asiye na uchungu kuhusu maendeleo ya familia iliyoachwa hivyo kutumia mali iliyoachwa kwa manufaa yake binafsi.
More Stories
IGP Sirro: Hatufungui kesi za madai, migogoro ya ardhi
Panyabuku waanza kubaini TB
Kigogo wa KKKT Kaskazini afariki dunia