September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Risasi za polisi zatikisa Mahakama ya Kisutu

Spread the love

RISASI za moto zimesikika na kushitua ngoma za masikio ya wengi. Ni mchana wa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya askari wa Jeshi la Magereza kuamua kuzifyatua risasi za moto hewani, lengo likiwa ni kuwatanya ndugu wa watuhumiwa wa Ugaidi waliofika mahakamani hapo kuwalaki wapendwa wao, anaandika Faki Sosi.

Kesi iliyozua taharuki hiyo ni ile inayomkabili Sheikh Ahmed Farid Hadi, Kiongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), na wenzake.

Askari hao, walirusha risasi moja hewani, walipokuwa wanaingia katika mahakama hiyo na baadaye kurusha risasi mbili wakati wakiondoka na watuhumiwa.

Walirusha risasi hizo kwa madai ya kutaka kuwasambaratisha ndugu wa watuhumiwa hao waliokaa kando ya barabara, wakipaza sauti na kusema,  “Allah Akbari” yaani, Mungu ni Mkubwa.

Mmoja kati ya askari aliyekuwepo katika msafara huo, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo alidai kuwa watu walikuwa wakiusogelea msafara wao.

error: Content is protected !!