Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Ripoti ya uchunguzi sakata la Mto Mara yapingwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Ripoti ya uchunguzi sakata la Mto Mara yapingwa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeombwa kufanya upya uchunguzi upya ili kubaini chanzo cha kuchafuka kwa maji ya Mto Mara na kufa kwa samaki mtoni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa katika nyakati tofauti, siku tatu baada ya Kamati Maalumu ya Kitaifa iliyoundwa na Serikali kuchunguza sakata hilo, kutoa riopoti yake iliyoeleza chanzo cha uchafuzi huo kuwa ni kinyesi na mikojo ya ng’ombe.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof. Samuel Manyele

Akizungumza na MwanaHalisi Online leo tarehe 22 Machi, 202, Msemaji wa Kisekta wa Chama cha ACT-Wazalendo, katika Wizara ya Maji na Mazingira, Ndolezi Petro, amesema majibu ya uchunguzi wa kamati hiyo hayaingii akili.

Kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kukinzana na matokeo ya uchunguzi uliofanywa awali, iliyosema chanzo chake ni uwepo wa mafuta na grisi, yaliyopelekea ukosefu wa hewa ya oksijeni na kupelekea samaki hao kufa.

“Juzi tumepata ripoti nyingine inasema chanzo cha maji kuchafuka na samaki kufariki ni uwepo wa kinyesi na mikojo kutoka kwa ng’ombe. Huu ni upotoshaji mkubwa kwa umma, sababu hizo taarifa mbili zimekinzana,” amesema Ndolezi.

Ndolezi amesema, ACT-Wazalendo kinapendekeza uchunguzi mpya ufanywe na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kwa kushirikiana na maabara huru za watu binafsi, ili majibu sahihi yapatikane kwa ajili ya kubaini chanzo na muarobaini wake.

“Sisi tunapendekeza zoezi la uchunguzi akabidhiwe mkemia mkuu, apatiwe sampuli akapime aje na matokeo halisi tujue nini kimejiri, ni vyema Serikali itoe vibali huru kwa sekta binafsi hasa maabara za kuaminika, ziweze kufanya uchunguzi, mwisho wa siku tupate majibu linganifu tufahamu nini tatizo,” amesema Ndolezi.

Ombi hilo pia lilitolewa na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, ambaye aliiomba Serikali iunde tume huru ya kuchunguza sakata hilo.

“Tunaitaka Serikali itafute au iunde timu nyingine huru, yenye watu huru hata wakiwa wachunguzi wa kimataifa wachunguze sababu hili jambo linahusu maisha ya watu. Tutafute maabara huru hata za nje ya nchi, ichunguze kisha iwaambie Watanzania ukweli ili kuondoa hofu,” alisema Heche.

Aidha, Heche alimuomba Rais Samia Suluhu Hassan, amfukuze kazi Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, kwa kushindwa kuwajibika katika suala hilo.

“Rais amfukuze kazi Waziri Jafo kwa kudanganya Watanzania wote, sababu jambo ili ulipeleke kwa umma lazima uaminike. Watu wamekataa hili jambo, kila mtu anashangaa hajawi kuona kinyesi cha ng’ombe kikiuwa samaki,” amesema Heche.

Heche ameiomba Serikali ichukue hatua za dharura kuwanusuru wananchi wanaotumia maji ya mto huo, kwa kuwapelekea maji safi na salama ya kutumia wakati ufumbuzi wa sakata hilo ukitafutwa.

Naye Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amekosoa matokeo ya ripoti hiyo akisema “toka awali tulishasema kwamba iundwe tume huru kwa ajili ya kuchunguza yale masuala, lakini tunasikitika matokeo yamekuja tofauti.”

“Hatuwezi kupinga moja kwa moja, lakini yanashangaza kuona kwamba inasemekana vinyesi vya wanyama ndiyo inasababisha hizo changamoto. Hoja yetu ni kwa kiasi gani ukubwa wa vinyesi vinaweza kupatikana kwenye eneo hilo ambao hakuna ufugajiu mkubwa kuliko maeneo mengine?” amehoji Olengurumwa.

Maoni hayo yametolewa ikiwa zimepita siku kadhaa tangu tarehe 19 Machi 2022, kamati hiyo kusema chanzo cha tatizo hilo ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof. Samuel Manyele alisema changamoto hiyo ilipelekea kuwepo kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni, pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto, hasa mimea vamizi kama vile maji na matete.

Prof. Manyele amesema mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara, hauhusiki na uchafuzi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!