September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ripoti ya Polisi sakata la Hamza, yaibua maswali magumu

Hamza Mohamed, aliyefyatulia risasi Polisi na kuwaua

Spread the love

 

RIPOTI ya awali ya uchunguzi wa tukio la mauaji ya maofisa watatu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi, pamoja na mshukiwa wa kujitoa mhanga, Hamza Mohammed, imeibua mjadala mwingine mpya, miongoni mwa jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mjadala wa sasa, unahusu ripoti ya uchunguzi kushindwa kujibu maswali kadhaa ambayo yalijitokeza baada ya shambulio hilo, lililotokea mchana wa tarehe 25 Agosti 2021, ikiwamo “umiliki halisi wa silaha” iliyotumiwa na Hamza, kuwashambulia maofisa wawili wa polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, juzi Alhamisi, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Cammilius Wambura, hakutaja aina ya silaha aliyoitumia Hamza kuwashambulia maofisa hao wa Polisi wala alivyoimiliki.

Kabla ya Wambura hajazungumza na waandishi wa habari juzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, alinukuliwa akisema, Hamza aliwafyatulia risasi polisi wawili kwa kutumia bastola, kisha akawapokonya bunduki zao na kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa, ambako alimuuwa mlinzi.

Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wanafamilia wa Hamza, aliyejitambulisha kwa majina ya Abdulrahman Hassan, ambaye ni shemeji wa mshambuliaji huyo aliyekuwa akijihami na silaha, alikuwa akimiliki bastola kwa sababu ya maeneo aliyokuwa akifanya kazi huko porini.

Alisema, Hamza ambaye aliuawa kwenye tukio hilo lililotokea makutano ya barabara ya Kinondoni na Kenyatta jijini Dar es Salaam, “alitumia muda wake mwingi kwenye shughuli zake za migodini na alikuwa mtu mwema sana.”

Lakini taarifa ya Wambura ilisema, aliwahi kumiliki mgodi huko nyuma, kinyume na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na familia yake na watu wengine wanaomfahamu.

Undani wa habari hii soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumamosi tarehe 4 Septemba 2021 ikiwemo kujua alichokisema Kamishna Wambura baada ya kuulizwa jana Ijumaa maswali kadhaa ikiwemo umiliki wa bastola aliyoitumia kuwaua askari hao.

error: Content is protected !!