RIPOTI ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limeiweka kwenye mazingira magumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuonesha chama hicho kutoa lugha ya uchochezi katika kampeni zake za Ubunge wa Jimbo la Kinondoni. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Kinondoni, Ismail Murilo iliyotoka kwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa huo, inaonyesha katika kampeni ya Chadema wasemaji wake wameeleza kuwa hawaogopi jeshi hilo na kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewasababishai dhiki watanzania.
Kamanda Murilo amesema katika kampeni zilizofanyika Februari 10, mwaka huu zilikuwa zikizungumzia masuala mengi licha ya ripoti hiyo kuwasilishwa kwa eneo dogo kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imewataja wazungumzaji ni pamoja na Joseph Kasambala, Ally Hemed, Mangweshi, Makongoro Mahanga, Boniface Jacob, Meya wa Ubungo, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe na Easter Bulaya, Mbunge wa Bunda.
Wakati huohuo, ripoti hiyo ilieleza kuwa chama cha wananchi (CUF) kilifanya mkutano eneo la Kigogo ambapo wawaeleza wananchi kuwa wamchague mgombea wao na kwamba polisi wawe wapole. Wasemaji ni pamoja na Kilwa, Jalia Bahati, na Miraji.
Pia CCM nacho kimefanya Mkutano wake eneo la mzimunini, wasemaji walikuwa ni Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtela, Joseph Msukuma, Mbunge wa Geita pamoja na Professa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega, pamoja na Feustine Ndungulille ambao waliwataka wananchi kumpgia kura mgombea wao.
Leave a comment