Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Ripoti ya Kamati kuhusu Bodi ya Mikopo yachafua hali ya hewa bungeni
HabariKitaifa

Ripoti ya Kamati kuhusu Bodi ya Mikopo yachafua hali ya hewa bungeni

Spread the love

 

RIPOTI ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kuhusu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kupinga maelekezo ya Waziri imechafua hali ya hewa bungeni baada ya kubaini kuwa hakukuwa na ukwamishaji wowote. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hivi karibuni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, alinukuliwa akieleza kuwa Bodi ya Mikopo inazuia Timu yake ya uchunguzi kutekeleza majukumu yake na kwamba huenda inataka kuficha madudu.

Akiwa bungeni pia alitoa kauli ya kuishutumu bodi ya mikopo kwa kueleza kuwa upinzani anaoupata baada ya kuunda kamati ya uchunguzi unamfanya aamini kuwa Bodi ya Mikopo ina matatizo.
“Mimi nilichogundua, baada ya kuunda hii Tume, Kamati sio Tume, resistance ambayo ilikuwepo ya kuzuia isifanye kazi imenishawishi kwamba huenda kuna madudu makubwa sana katika Bodi…” alisema Mkenda.

Akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kuhusu sakata hilo bungeni leo Jumatatu tarehe 7 Novemba, 2022, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, amesema Kamati “haijapata ushahidi wowote unaoonesha kwamba Bodi ya Mikopo ilileta kiburi na kukwamisha utendaji wa Waziri.”

Badala yake amesema baada ya hadidu za rejea kuwasilishwa Bodi ya Mikopo, Kamati ya Waziri imeanza na kuendelea kufanya kazi, jambo linaloashiria kutekelezwa kwa maelekezo ya Waziri.

Hata hivyo amesema wamebaini kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano na mahusiano ndani ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na baina ya Wizara na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini.

Matokeo ya ripoti hiyo yamewafanya baadhi ya wabunge kuhoji sababu ya Waziri kufikisha jambo hilo bungeni kama hakukuwa na tatizo huku wengine wakimtaka ajitafakari kama bado anatosha katika nafasi hiyo au aachie ngazi.

Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamis Kigwangala, amesema Waziri amelidanganya bunge hivyo anapaswa kuomba radhi na kujitafakari kama anafaa kuendelea na wadhifa huo.

Baada ya kauli hiyo ya Kigwangala Mbunge wa Bunda, Mwita Gitere alisisimama na kumpa taarifa kuwa anapaswa kutangaza mgongano wa maslahi kwani alishawahi kuwa na mgogoro binafsi na Profesa Mkenda kipindi wakiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mgogoro wa Kigwangala na Mkenda uliwekwa hadharani na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli, ambapo aliweka wazi kutoelewana baina ya Waziri (Kigwangala) na Katibu Mkuu wake (Mkenda) na kuwataka kumaliza tofauti zao.

Baada ya Kigwangala kupewa taarifa hiyo, Spika Dk. Tulia Akson alipigilia msumari kuwa ni kweli mbunge huyo ameonesha upande hata kabla ya ripoti kuwasilishwa kwa kumuhukumu Mkenda kupitia mitandao ya kijamii na kumtaka ajielekeze kwenye hoja za kamati.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda alisimama na kuhoji sababu za Bodi ya Mikopo kuilipa Kamati ya uchunguzi inayowachunguza.

“Mimi ninaona kuna tatizo inakuaje Bodi ya Mikopo amabyo inachunguzwa inawalipa Kamati ambayo inawachunguza,” amesema Mwakagenda.

Hata hivyo Mwakagenda amesema haoni kama Waziri alidanganya bunge wala kuishtaki Bodi ya Mikopo Bungeni bali aliomba asaidiwe ili nchi iweze kufanya kazi vizuri.

“Kukosea kupo lakini hata kama wanasema amelidanganya bunge mimi sioni kama amelidanganya bunge vinginevyo wewe Mh. Spika usingetoa nafasi ya kufanya hivi,” amesema Mwakagenda.

Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, amesema haiwezekani bunge limfundishe Waziri namna ya kufanya mawasiliano na watendaji wake, “kama tumeamua kufunika kombe mwanaharamu apite lakini ukweli utabaki waziri na timu yako panga mawasiliano vizuri hatutaki kuchafuliwa hali ya kisiasa,” amesema Kingu.

Kasalali Maageni, jambo hilio ambalo tunalijadili humu la mawasilinao yasiofuata taratibu ndilo limemfanya Spika aunde tume na jambo hili ndilo tatizo la msingi linalofanya vijana kukosa mikopo.

Akichangia taarifa hiyo ya kamati Profesa Mkenda amesema hakusema
“Sikuja kuishtaki bodi humu sina haja ya kuishtaki bodi,” amesema na kuongeza kazi imeanza tangu tarehe 31 na Kamati inapata ushirikiano mkubwa kutoka bodi.

Wakati Mkenda akiendelea kuchangia Mbunge Kasalali Mageni alisimama na kuomba kumpa taarifa kuwa msingi wa bunge kutaka Kamati iwahoji ni baada ya kuonekana kuna matatizo.

“Mnavyosema hakuna tatizo inaonesha hii kamati haikuwa na haja ya kufanya hiyo kazi, wala hatuna haja ya kuendelea kujadili hii ripoti,” amesema.

Hata hivyo Mkenda likataa taarifa hiyo na kabla ya kuendelea kuchangia Mbunge Elibariki Kingu aliomba kumpa taarifa na aliposimama alihoji sababu ya jambo hilo kuletwa bungeni kama kulikuwa hakuna tatizo.

Profesa Mkenda amejibu hoja hiyo kuwa hakuwa ameridhika na kasi ya utekelezaji na akatoa onyo hadharani na si bungeni na kwambaa baada ya onyo hilo kazi ilianza kwa kasi kubwa.

“Na ndiyo jukumu langu nilizungumza in public na labda ni nukuu lisema atakayenikwamisha kamati hii nitamla kichwa ipo ndani ya uwezo wangu na nilizungumza hivyo na kamati ilianza kazi,” amesema Mkenda.

jambo hilo hakulizungumza bungeni bali ilikuwa nje ya bunge “na narudia nilichosema kwamba wakiendelea nitakula kichwa”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

Kitaifa

Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo

Spread the love  SERIKALI nchini Tanzania imetenga eka 10 kwa kila kijana...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

error: Content is protected !!