May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ripoti ya CAG Zanzibar yamuibua Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

 

UBADHIRIFU ulioibuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Zanzibar, kwenye mwaka wa fedha wa 2019/2020, umemuibua Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Leo Jumapili tarehe 23 Mei 2021, Rais wa Zanzibar, Dk.Hussein Mwinyi, alikabidhiwa ripoti hiyo  na Kaimu CAG, Dk. Othman Abbas Ally, katika  Ikulu ya Zanzibar.

Katika ripoti hiyo, CAG alibaini ubadhirifu wa fedha katika baadhi ya wizara, taasisi na mashirika ya umma.

 

Akizungumzia ripoti hiyo, Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo, kilichoshiriki katika uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), iliyoko madarakani,   amesema ufisadi ulioibuliwa hauvumiliki.

“Nimesikiliza Taarifa hii ya CAG Zanzibar. Ni hatari kabisa. Kiwango cha udokozi, wizi, ubadhirifu na ufisadi hakimithiliki,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Awali akiwasilisha ripoti hiyo, Dk . Othman alisema ukaguzi uliofanywa na CAG umebaini fedha za Serikali zaidi ya Sh. 5 Bil. hazijulikani zilipo.

Mbali na ubadhirifu huo, Dk. Othman alisema ukaguzi huo ulibaini madudu kwenye Wizara ya Kilimo visiwani humo, uliotokea katika ununuzi wa mbolea aina ya Urea tani 740, uliogharimu Dola za Marekani 279,720.
Pia, CAG alishindwa kuthibitisha ununuzi wa mbolea ya Urea tani 454 ulioghrimu Sh. 24,113,630, baada ya kukosa nyaraka za ununuzi na mapokezi yake.

 

Vilevile, ukaguzi wa CAG ulibaini bakaa ya fedha Sh.106.12 milioni, zilizopaswa kurudishwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Zanzibar, hazikurudishwa.

Dk. Othman amesema ukaguzi huo umebaini tofauti ya Sh. 579.4 milioni, iliyotokana na kutokuwiana kwa taarifa za fedha za wizara hiyo, ambapo ripoti yake ya jumla inaonesha Sh. 4.69 bilioni wakati taarifa ya mfumo wa matumizi ya fedha  za miradi ya maendeleo ikionesha Sh  4.17 bilioni.

Katika Wizara ya Fedha na Mipango, ukaguzi huo umebaini kodi ya ongezeko la thamani dola 928,107, haikukatwa katika matumizi ya dola 5.15 milioni yaliyofanyika kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

 

error: Content is protected !!