Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya CAG: Ukwapuzi mabilioni TEITI yadaiwa bungeni
Habari za Siasa

Ripoti ya CAG: Ukwapuzi mabilioni TEITI yadaiwa bungeni

Jesca Kishoa
Spread the love

 

TAARIFA ya uchunguzi maalumu wa upotevu wa fedha kiasi cha Sh. 90 Bilioni, aliyonayo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inadaiwa bungeni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jesca Kishoa, mbunge asiye na chama bungeni, ameiomba Ofisi ya Spika, iiagize serikali kupeleka bungeni taarifa ya CAG, kuhusu ukaguzi maalum wa fedha hizo ambazo hazijulikani zilipo.

Kishoa ametoa ombi hilo leo Alhamisi tarehe 29 Aprili 2021, wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022, jijini Dodoma.

Mbunge huyo amesema, sakata hilo liliibuliwa katika Ripoti ya Taasisi ya Uhamasishaji na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), ambayo ilidai kwamba fedha zaidi ya Sh. 90 Bilioni hazijulikani zilizpo.

“Nimepitia ripoti za TEITI 10, toka mwaka 2009 hadi 2019, kuna mambo yanasikitisha kweli, TEITI wameripoti kuna risiti za malipo kutoka makampuni ya madini kwenda serikalini hazionekani,na wanasema zaidi ya fedha Sh. 90 Bil. hazina maelezo ziko wapi, hizi sio taarifa zangu, ni taraifa kutoka TEITI,” amesema Kishoa ambaye ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema waliotimliwa.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Kishoa amesema baada ya ripoti hiyo kuibua suala hilo, CAG alipewa kazi ya kufanya ukaguzi maalum, lakini matokeo ya ukaguzi huo hayajawekwa hadharani.

“CAG alipewa kazi maalum kuchunguza ripoti ya saba na nane, kuangalia fedha hizi zimekwenda wapi, nataka nikujulishe naibu spika, ripoti hii tangu CAG ameifanyia kazi imefichwa makwapani. Hatujaiona na hatujui iko wapi.”

Kufuatia sakata hilo kutojulikana hatma yake, Kishoa amesema “iko haja naibu spika kupitia kiti chako kama itakupendeza, uitake serikali ile ripoti ambayo CAG aliikagua akairudisha wizarani, iletwe hapa bungeni, wabunge tuihoji na tuipitie kwa pamoja.”

Mwanasiasa huyo ameishauri serikali, itunge sheria itakayompa mamlaka CAG kukagua fedha zinazolipwa serikalini kutoka katika kampuni binafsi.

“Zaidi ya Sh. 90 Bilioni hazina maelezo yoyote, naishauri serikali kuna kila sababu ya kutunga sheria kumpa mamlaka CAG aweze kuwa na mamlaka ya kukagua pesa zinazotoka kwenye kampuni na pesa zinazolipwa serikalini,” amesema Kishoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!