September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ripoti uchunguzi soko la Kariakoo kutua kwa Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RIPOTI ya uchunguzi wa ajali ya moto katika Soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam, inatarajiwa kuwasilisha kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Gabriel Mushi (endelea…)

Moto huo uliteketeza sehemu ya juu ya soko hilo, usiku wa tarehe 10 Julai 2021 na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Jumapili,tarehe 12 Septemba 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Mbali na ripoti hiyo, Msigwa amesema maandalizi ya ukarabati wa soko la Kariakoo yanaendelea lengo ni kuhakikisha soko hilo linatoa huduma za kimataifa kwa saa 24 na kwa mazingira rafiki na salama kwa mtu yeyote.

Amesema lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha baada ya ajali iliyotokea soko hapo lirudishwe katika hadhi ya kimataifa.

“Soko linatakiwa kutoa huduma kwa saa 24 kama ilivyo mengine duniani hasa kwa kuzingatia mazingira mazuri na kuondoa mazingira hatarishi,” amesema.

Gerson Msigwa, Msemaji wa Serikali

Tarehe 27 Julai 2021, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio hilo la moto kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hayo, Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas.

Majaliwa alisema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais Samia kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.

“Naahidi mbele yako mwenyekiti kuwa Serikali nimeridhishwa na taarifa mliyo nikabidhi leo na mapendekezo yote mliyoyatoa yatazingatiwa.

Jumapili tarehe 11 Julai, 2021 Majaliwa alipotembelea na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto katika soko la kimataifa la Kariakoo alitangaza kamati ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.

Tarehe 21 Julai, 2021 Majaliwa aliongeza siku saba kwa kamati aliyoiunda kuchunguza kuungua kwa soko la Kariakoo hadi Julai 25, mwaka huu.

error: Content is protected !!