Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ripoti: Chanjo za Corona zinaweza kuathiri hedhi
Kimataifa

Ripoti: Chanjo za Corona zinaweza kuathiri hedhi

Spread the love

 

WATAALAM kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya barani Ulaya (EMA) wameonya kuwa baadhi ya chanjo za Covid 19 zinaweza kusababisha akina mama kutokwa na damu nyingi katika siku zao ‘hedhi’.
Wataalamu hao wametaka ugunduzi huo uongezwe katika orodha ya uwezekano wa athari inayoweza kutokea iwapo mtu akipatiwa chanjo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa ya shirika hilo limetaja chanzo za Pfizer na Moderna, kuwa zimeonesha athari hizo na hasa katika chanjo ya pili au zile za nyongeza.

Kwa mujibu ya mamlaka hiyo, mchakao wa hedhi ambayo inafanyika kwa kuongezeka kiwango cha utokaji damu au kufanyika kwa muda mrefu kinaathiri ustawi wa afya ya mwanamke husika. “Hali hiyo imebainika katika chunguzi kadhaa za kitabibu,” EMA ilisema.

Katika hitimisho lake mamlaka hiyo imesema angalau kumekuwa na uwezekano kwamba kiwango kikubwa cha kutokwa na damu za hedhi ni athari inayohusishwa na aina hizo za chanjo.

Msemaji wa Moderna amesema kampuni yake ina taarifa za ripoti ambazo zinahusisha chanjo ya “dysmenorrhea” au maumivu yenye kuhusiana na kipindi cha hedhi.

“Lakini hata hivyo bado hawajagundua athari zenye kuhusiana na chanjo ya Moderna, Spikevax”.

Kwa upande mwingine kampuni ya BioNTech inayotengeneza chanjo ya Pfizer haikupatikana mara moja kueleza kuhusu ripoti hiyo.

Hata hivyo, pia mamlaka EMA imesema katika ripoti ya uchunguzi wake hakuna ushahidi wa wazi unaoonesha matatizo ya hedhi yanayowapata baadhi ya kina mama kuwa yana athari yoyote katika suala la afya ya uzazi na uzazi wao.

Kikosi kazi cha dharura cha mamlaka hiyo kimesema chanjo za mRNA hazisababishi matatizo ya ujauzito, akina mama wajawazito au watoto wao.

Matukio ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi yamekuwa yakifanyiwa uchunguzi katika ngazi ya kitaifa na Ulaya kwa ujumla wake tangu ripoti za kwanza kuonekana kati ya wanawake waliochanjwa.

Matatizo ya hedhi kwa akina mama yanaweza kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali zao kiafya, msongo wa mawazo na uchovu.

Mamlaka za afya zimetoa tahadhari baada ya ugunduzi kuonesha visa hivyo vimeripotiwa baada ya kutokea mikasa ya maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!