Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti CAG yabaini ubadhirifu Wizara ya Kilimo Z’bar
Habari za Siasa

Ripoti CAG yabaini ubadhirifu Wizara ya Kilimo Z’bar

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi wa Fedha za Serikali Visiwani Zanzibar (CAG), Dk. Othman Abbas Ali, amemefichua ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi katika wizara ya kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea). 

Akiwasilisha ripoti yake kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, CAG Othman amesema, jumla ya Sh. 1.3 bilioni hazijulikani zilipo, baada ya wizara hiyo kushindwa kuthibitisha matumizi yake.

Amesema, jumla ya Sh. 1.3 bilioni, zimepotea katika wizara hiyo, na kwamba ofisi yake, imeshindwa kuthibitisha matumizi yake.

Amesema, “tarehe  23 Juni 2020, wizara imefanya matumizi ya Sh.  1.3 bilioni  kwa ajili ya huduma mbalimbali. Lakini ukaguzi wangu haukupatiwa uthibitisho juu ya uwepo wa matumizi ya fedha hizo.”

Dk. Othman amesema, “nilipowauliza watu wa wizara  wanasema, fedha hazikuingia, lakini  mfumo  wa malipo unaonesha fedha zimetoka.”

Mbali na fedha hizo, kiasi cha Sh. 640.3 milioni, zilizotolewa na wizara hiyo, kwa ajili ya kuboresha huduma za uhifadhi, hazijulikani zilipo,  baada ya waliopaswa kupewa kukana kupokea.

“Ukaguzi wangu umebaini kukosekana kwa uthibitisho wa mapokezi ya kiasi cha Sh. 640.3 uliofanywa na wizara, ikiwa ni mgawo kwa lengo la uhifadhi na kuendeleza miradi ya maendeleo kwa jamii,” ameeleza CAG huyo.

Kaimu CAG Zanzibar, Dk. Othman Abbas Ali

Amesema, “wizara imesema, imewapa fedha hizi viongozi wa vijiji,  lakini nilipokutana na wanavijiji walikataa kupokea fedha hizo na hakuna uthibitisho wowote wa kupokewa fedha hizo na wanavijiji.

“Nimejaribu kuwasiliana na watu wa kilimo, lakini mpaka sasa, suala hili halijapatiwa ufumbuzi.”

Dk. Othman amesema pia, kwamba  ukaguzi wake,  umebaini uwepo wa tofauti ya Sh. 579.4 milioni, katika wizara hiyo, baada ya kutowiana kwa taarifa za fedha.

Amesema, fedha zilizotoka zilikuwa Sh. 4.6 bilioni, wakati zilizotumika ni Sh. 4.1 bilioni.

Amesema, lakini  fedha zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya kazi za miradi ya  maendeleo,  zilizoripotiwa na wizara  ni Sh. 4.1bilioni, jambo ambalo limefanya kuwapo kwa tofauti na ambayo ofisi yake, haikupata maelezo ya uwepo wake.

Dk. Othman alisema, wizara hiyo ilipoteza kiasi cha Sh. 55.6 milioni kutokana na kulipa watumishi wake, waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2017.

Katika hilo, Dk. Othman amesema, “ukaguzi wangu ulibaini uwepo wa matumizi ya Sh. 55.6 milioni,  zilizolipwa kwa watumishi ambao hawako kazini kwa muda mrefu. Kuna barua nimezionesha katika ripoti yangu, kuwasimamisha kazi,  zilizotoka 2017 kwa watumishi wawili.

“Lakini hadi leo wanalipwa mishahara, pia kuna barua za likizo walizopewa za bila malipo toka 2019 na bado fedha hizo zinaingia katika akaunti za watumishi hawa.”

Naye Rais Dk. Mwinyi, mara baada ya kupokea taarifa hiyo alisema, yaliyomo ndani ya ripoti, “yamenihuzunisha sana.”

Dk. Mwinyi alisema, ufisadi na matumizi mabaya yaliyogundulika na CAG yanathibitisha kuwa waliopewa nafasi ya kuwa viongozi wa umma, hutumia madaraka yao kujinufaisha binafsi.

Alisema, ripoti imeonyesha kuwapo kwa upotevu mkuwa wa fedha za serikali katika makusanyo na kwamba taasisi zilizopewa jukumu la kukusanya fedha zimeshindwa kufanya kazi hiyo.

1 Comment

  • Je kuna hatua za kisheria zjimechukuliwa? Au ni kuhuzunika tu kama kawaida? Dokta fanya kwa vitendo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!