July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rioba: CCM inawauzia wananchi mbuzi kwenye gunia

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu Mwenezi na Itikadi, Nape Nnauye wakisalimia wananchi

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu Mwenezi na Itikadi, Nape Nnauye wakisalimia wananchi

Spread the love

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano (SJMC),Dk.Ayoub Rioba amesema kitendo cha Chama Cha Mapinduzi kuwataza wagombea wa nafasi ya urais kushiriki midahalo sawa na kuuzia watanzania mbuzi kwenye gunia. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio Jijini Dar es Salaam kuzungumzia zoezi la wagombea hao kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.

Amesema kitendo cha uongozi kukataza wagombea kushiriki midahalo itawaathiri kwa kuwa mgombea sahihi anatakiwa achaguliwe na wananchi kwa kuwasikiliza katika midahalo na kuwapima na siyo CCM.

“CCM kukataza wagombea wao kushiriki katika midahalo itawaathiri sana na ni sawa na kuwauzia wananchi mbuzi kwenye gunia inatakiwa wagombea wajieleze kupitia midahalo ili wananchi wawapime na kuwachagua”amesema Rioba.

Kauli hiyo ya Rioba ambae pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa imekuja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu na Organezesheni na Chama hicho Dk.Mohamed Seif Khatib kusema wagombea wao hawezi kushiriki katika mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya CEO Roundtables.

Dk.Khatib akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema wagombea wao hawawezi kushiriki katika mdahalo huo hadi baada ya kupatikana mgombea mmoja ndipo watakubali kufanya mdahalo kwa kuwa wakifanya hivyo sasa hivi ni kuchanganya wanachama na wananchi utatoa nafasi ya wao kulumbana na kupakana matope.

Kwa mujibu tangazo hilo lilitolewa na taasisi hiyo inayoundwa na watendaji wakuu wa makampuni nchini mdahalo huo ulikuwa unalenga kuunda jukwaa huru ambalo litawezesha kipaumbele cha wapiga kura na maendeleo nyeti ya msingi yanayoikabili Tanzania.

error: Content is protected !!