March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ridhiwani Kikwete ‘apaniki’

Spread the love

RIDHIWANI Kikwete, Mbunge wa Chalinze ameishiwa uvumilivu. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Mbunge huyo kijana anaeleza kukerwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba ‘anakerwa’ na wanasiasa wanaohama vyama vyao na kujiunga na Chama Cha mapinduzi (CCM).

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ameeleza kuwa, maneno yanayosambazwa na kudaiwa yake  ni uzushi.

Amesema haki ya raia wa Tanzania kuhama chama ni ya kikatiba hivyo atakuwa mtu wa ajabu kupuuza hilo.

“Ikumbukwe Ndg. Watanzania wenzangu na hususani WanaCCM wenzangu, mapema mwanzoni  mwa waka huu 2018,
tarehe 22 niliutaarifu umma ukweli juu ya kile nilichokiita maneno ya kiuchonganisha yanayolenga kunigombanisha mimi na uongozi wa Chama Changu CCM.

“Kupitia ujumbe mdogo wa video nilikanusha juu ya maneno hayo kwamba  sikuyaandika mimi na wala sina uhusiano wowote na maneno hayo.
” Lakini la kushangaza baada ya miezi saba, jambo hilo linaibuka tena leo.” Amelalamika Ridhiwani.

Amesema, Januari 22 mwaka huu aliweka video akieleza kutofurahishwa na kitendo cha kulishwa’ maeno.

Anasema “sijawahi kusema wala kuandika maneno hayo, yanayolenga kukiambia chama na serikali yangu kupuuza hawa wanaohamia chama na Kupelekea kufanyika chaguzi za mara kwa mara.

“Nataka kuwahakikishia, kama Mwanasheria ninatambua haki aliyonayo raia Kikatiba. Sintokuwa tayari kusema neno ambalo litapotosha kiapo changu kama Mwanasheria ninayeheshimu Haki na Usawa katika Binadamu.”

Ridhiwani amesema kuwa, hahusiki na nomaneno yanayotengenezwa na kwamba, Watanzania wayapuuze.

error: Content is protected !!