September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Richard Mabala amkosoa Rais Magufuli

Spread the love

 

MWANDISHI mkongwe wa vitabu nchini, Richard Mabala amekosoa hatua ya serikali kuhamia Dodoma kama wamekurupushwa, anaandika Pendo Omary.

Mabala ameonesha kuwa, nia ya Rais John Magufuli la kuitaka serikali yake kuhamia Dodoma kabla ya mwaka 2020 kwa mkupuo ina kasoro ndani yake.

Tayari Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ametangaza kuhamia Dodoma Septemba Mosi mwaka huu ikiwa ni hatua ya kutekeleza agizo la Rais Magufuli na kuagiza wizara zote kufanya hivyo huku Wizara ya Elimu ikiitikia amri hiyo kwa haraka.

Akiandika katika ukurasa wake wa facebook Mabala ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu na masuala ya jinsia amesema “hivi suala la kuhamia Dodoma kwa mkurupuko kama vile tunafukuzwa na Simba siyo suala la kijinsia?

“Wako wafanyakazi wanawake wangapi ambao wanawalea watoto peke yao? Inabidi wawasimamie kwenda shuleni kila asubuhi na kuwapikia jioni na kuhakikisha wako vizuri?

“Wako wangapi ambao katika saa za jioni wanaendesha miradi mingine ili kupata pesa za kutosha kulea familia? Ukiwalazimisha hawa kuhamia Dodoma ndani ya wiki 2 ama sivyo wamejifukuzisha kazi, umewatendea haki?,” amehoji Mabala.

Miongoni mwa kazi za uandishi wa vitabu vya Mabala vilivyotumika katika Shule za Sekondari Tanzania ni pamoja na The Hawa Bus Driver na Mabala the Farmer.

Pia Mbobezi wa Uchumi nchini Profesa Honest Ngowi amekosoa  kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kwamba, baada ya serikali kuhamia Dodoma itauza majengo yake yote inayomiliki jijini Dar es Salaam.

“Wafanyakazi wengine watakwenda Dodoma, watakao baki wataingia kwenye hayo majengo. Bila shaka sioni Ikulu ikiuzwa, sioni BOT ikiuzwa.

“Kitakachofanyika kwa mtazamo wangu pengine hizo zitakuwa ni ofsi ndogo,” amesema Ngowi wakati akihojiwa leo na radio Deutsche Welle Idhaa ya Kiswahili.

error: Content is protected !!