Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Rice 360 yawajengea uwezo wafanyakazi DIT
Habari Mchanganyiko

Rice 360 yawajengea uwezo wafanyakazi DIT

Spread the love

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Rice ya nchini Marekani (Rice 360 Institute for Global Health) wanaendesha mafunzo kwa watumishi wa DIT ya kuwaongezea uwezo ili bunifu au kuboresha mawazo yanayozalishwa na wabunifu yaweze kujibu mahitaji ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mafunzo hayo ya wiki moja yakiwa na mada mbalimbali yameanza leo Jumatatu tarehe 7 Machi 2022 jijini Dar es Salaam.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba amesema, haya ni mafunzo muhimu sana kwa wafanyakazi na kwa jamii ambayo inaitegemea DIT ili kutatua matatizo mbalimbali yanayowazunguka.

Amesema, “mafunzo haya ni kwa ajili ya wafanyakazi wetu ili kuongezewa uelewa wa namna bora ya kusanifu mitambo na vifaa mbalimbali vya uhandisi hususan vifaa tiba.”

Profesa Ndomba amesema, ili kuweza kufanikisha haya ni lazima kushirikiana na vyuo mbalimbali na na kwamba wameona Taasisi ya Rise 360 ni sahihi kabisa, na kuongeza, “licha ya wafanyakazi wetu kusoma nje ya nchi, lakini mafunzo haya yatatusaidia kutuongezea ujuzi kwani teknolojia inapanuka kila kukicha.”

“Pale kwetu tuna karakana ya kuzalisha vifaa tiba na baada ya mafunzo haya tutakwenda kuboresha bunifu zetu na badala ya kuagiza vifaa kutoka nje ya nchi, sasa tutakuwa tunavizalisha hapa hapa kwetu na kuisaidia jamii na Serikali,” amesema Profesa Ndomba.

Profesa Ndomba amesema, tumekwisha kutengeneza ventilators lakini baada ya mafunzo haya tutakwenda kuiboresha zaidi “ili iweze kwenda kukidhi mahitaji ya wagonjwa na hii si kwa wagonjwa tu wa COVID-19 lahasha, ni kwa kusaidia wagonjwa kuweza kupumua kwani magonjwa haya yapo mengi.”

Amesema DIT imeingia makubaliano ya awali na Hospitali za Taifa ya Muhimbili (MNH), Aga Khan, Amana na CCBRT ambazo ni wadau muhimu kwa kutengeneza vifaa vyao DIT iwauzie.

“Sisi DIT tumejipambanua kwenda kutatua matatizo ya jamii na wadau wetu wa kwanza ni hizi hospitali na tunafanya matengenezo ya vifaa mbalimbali walivyonavyo na ndiyo maana tukaingia nao makubaliano,” amesema.

Naye Julia Jenjezwa, Meneja Usanifu wa Atamizi ya DIT (DIT Design Studio) amesema, wanataka kubadilika kutoka kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo hasa Taifa inapokumbwa na majanga p, lazima tubuni au kuanzisha mambo yanayokwenda kutatua matatizo ya wananchi.

“Vifaa tunavyobudi au mawazo yanayoanzishwa na wahadhiri na wanafunzi wao, yanapaswa kujibu matatizo ya wananchi. Tuondoke kwenda dhana ya nadhalia kwenda kwenye vitendo na hiki ndicho wananchi wanataka,” amesema Julia ambaye ni Mzimbambwe.

“Pale DIT tuna studio mbalimbali ya kutengeneza vifaa na kupitia mafunzo haya sasa, yatawajengea uwezo ili kwenda kuzalisha wanafunzi wenye kutatua matatizo ya jamii,” amesema.

Julia amesema, katika kipindi cha wiki moja cha mafunzo, washiriki watakwenda maeneo mbalimbali kama Hospitali ya Amana, Soko la Kisutu na mitaani kuangalia matatizo yaliyopo huko kisha watarudi na kuyatafutia ufumbuzi.

“Tutawafundisha wazo kulibadili kuwa suluhisho kwa jamii. Tunahitaji kubadili mitalaa ili iweze kwendana na matatizo ya Watanzania hasa kuwa na wahitimu waliokidhi viwango vya kutatua matatizo ya wananchi,” amesema Julia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Elimu na Mhadhiri wa Taasisi ya Rice 360, Dk. Ashley Taylor amesema, ushirikiano baina yao na DIT utakuwa na manufaa makubwa kwani watajengeana uwezo wa kwenda kukabili matatizo yaliyopo kwenye jamii.

“Tunahitaji kuwa na mchango kwenye jamii kwa kuangalia matatizo yanayowakabili wananchi na kubuni au kuanzisha bunifu zitakazokwenda kujibu au kuwa suluhisho na ndiyo maana tumekutana na wafanyakazi ambao nao watakwenda kukutana na wanafunzi,” amesema Dk. Taylor.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!