Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Reli ya kisasa Tabora-Kigoma yanukia
Habari Mchanganyiko

Reli ya kisasa Tabora-Kigoma yanukia

Reli ya kisasa ya SGR
Spread the love

 

SERIKALI imesema ipo mbioni kuanza utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Kigoma na hatimaye kuiunganisha na nchi za Burundi, Rwanda na DRC. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 12, 2022 na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC, Masanja Kadogosa wakati wa uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa SGR kipande cha Makutupora-Tabora.

Kadogosa amesema wapo kwenye utaratibu wa kutafuta msimamizi wa mradi huo ambao baadae itaunganishwa na na kufika hadi Uvinza.

Amesema kutokea Uvinza itaunganishwa hadi Msongati Kitega-Uvira-Kindu, “na sisi tulishapata tenda ya awali ya kumpa msimamizi wa mradi.”

“Reli yetu itabeba abiria lakini biashara yetu ni mizigo na mzigo wetu ni madini ya Nikeli , Copper, Lithium, na bati ambayo ni mazito kweli kweli na usafiri unaofaa ni reli,” amesema.

Amesema reli hiyo ni ya uzito wa Excel 35 ambapo behewa moja lina uwezo wa kubeba hadi tani 120.

“Vipande hivi vilikuwa muhimu sana katika ujenzi wetu na hii ndoto ilikuwa mbali na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ametutimizia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!