Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Michezo Rekodi kuipa Simba kiburi dhidi ya Kaizer Chiefs
MichezoTangulizi

Rekodi kuipa Simba kiburi dhidi ya Kaizer Chiefs

Spread the love

 

KUELEKEA mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, Simba inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na rekodi nzuri waliyoiweka kwenye kundi A baada ya kumaliza kama vinara kwenye masimao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu

Simba ambayo kwa sasa ipo nchini Afrika Kusini itashuka Uwanjani kesho kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza war obo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaochezwa majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanakwenda kuanzia ugenini mara baada ya kumaliza vinara kwenye kundi A, wakiwa na pointi 13 mbele ya mabingwa watetezi taji hilo la Afrika, klabu ya Al Ahly, As Vita pamoja na El Merreikh kutoka Sudan.

Simba inaingia kwenye mchezo huo huku kocha wa Didier Gomes akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwa kupata matokeo ya ushindi kutokana na rekodi nzuri za michezo ya ugenini kwenye michuano hiyo kiasi cha kutaka kila mtanzania na washabiki wa Simba kujivunia timu hiyo.

“Tunafuraha kucheza huo mchezo tumeusubiri kwa muda mrefu na itakuwa mechi ngumu, tutacheza kwa tahadhari na kujitolea,  tunataka kuwafanya watanzania na mashabiki wa simba kujivunia.” Alisema Didier

Katika michezo mitatu ya Simba iliyocheza hatua ya makundisafu yao ya ulinzi imeruhusu bao moja kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly uliochezwa kwenye Uwanja wa Al Salam na Simba kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0.

Licha ya kuwa na safu bora ya ulinzi lakini Simba pia imekuwa na safu bora ya ushambuliaji ambao katika michezo sita imepachika jumla ya mabao 9.

Kikosi cha Simba

Pia katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Simba imefanikiwa kupata matokeo katika michezo ya ugenini kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo dhidi ya AS Vita na sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya El Merreikh.

Kaizer Chiefs wao wamemalizika kwenye nafasi ya pili kundi C, wakiwa na pointi 9, nyuma ya Wydad Casablanca waliokuwa kwenye nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 13.

Katika michezo sita waliocheza Kaizer Chiefs kwenye kundi C, wamefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili, sare mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja, huku wakifanikiwa kupachika mabao 5 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara sita.

Simba imetua Afrika Kusini ikiwa na kikosi cha wachezaji 25 na tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo huo ambao marudiano utachezwa Dar es Salaam Tarehe 22 Mei 2021, kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

error: Content is protected !!