Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo Refa wa Yanga na Prisons, apewa mechi ya watani wa jadi
Michezo

Refa wa Yanga na Prisons, apewa mechi ya watani wa jadi

Emmanuel Mwandemba
Spread the love

 

EMMANUEL Mwandemba kutoka Arusha, ndiye atakayekuwa mwamuzi wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 11 jioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu utapchezwa Jumamosi tarehe 8 Mei, 2021, utasimamiwa na waamuzi wanne tofauti na mchezo uliopita ambao ulikuwa na waamuzi Sita na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Mwandemba ambaye atakuwa kati siku ya mchezo huo, alichezesha mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Tanzania Prisons ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1.

Kwenye mchezo huo, Mwandemba alitoa kadi nyekundu kwenye dakika ya 81 kwa beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona baada ya kufanya madhambi.

Waamuzi wengine kwenye mchezo huo ni, Frank Komba kutoka Dar es Salaam, ambaye atakuwa msaidizi namba moja na Hamdani Saidi kutoka Mtwara, atakuwa msaidizi namba mbili huku Mwamuzi wa akiba ni Ramadhani Kayoko kutoka Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!