July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Refa Mwandembwa apewa tena Rungu, mechi Simba na Yanga

Spread the love

EMMANUEL Mwandembwa kutoka Arusha, ndiye atakayekuwa mwamuzi wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 11 jioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu utapchezwa Jumamosi tarehe 3 Julai, 2021, utasimamiwa na waamuzi wanne tofauti na mchezo uliopita ambao ulikuwa na waamuzi Sita na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Mwandembwa anarudi kuwa mwamuzi kwenye mchezo huo, mara baada ya mchezo wa Mei 8 kuahilishwa, ambapo pia alipangwa kama mwamuzi wa kati.

Mwamuzi huyo ndiye aliyecheza mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi, kati ya Yanga na Tanzania Prisons ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1.

Kwenye mchezo huo, Mwandemba alitoa kadi nyekundu kwenye dakika ya 81 kwa beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona baada ya kufanya madhambi.

Waamuzi wengine kwenye mchezo huo ni, Frank Komba kutoka Dar es Salaam, ambaye atakuwa msaidizi namba moja na Hamdani Saidi kutoka Mtwara, atakuwa msaidizi namba mbili huku Mwamuzi wa akiba ni Ramadhani Kayoko kutoka Dar es Salaam.

error: Content is protected !!