September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Real Madrid yashusha mvua ya mabao

Spread the love

TIMU ya Real Madrid imeitandika Celta Virgo mabao 5-2, jana tarehe 12 Septemba, 2021 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu liliopo jijini Madrid Hispania. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo … (endelea).

Katika mchezo huo ambao miamba hao wa Los Blancos  kuibuka na ushindi huo mnono, mshambuliaji wake, Karimu Benzema akifunga mabao matatu (hat-trick), Vinicius Junior akifunga bao moja huku kijana mpya kwenye kikosi hicho, Eduado Camavinga naye aliikisa nyavu mara moja.

Benzema jana alikuwa katika kiwango bora pamoja na kijana mpya Camavinga ambao walijitoa ili kupata ushindi ambao ulikuwa ni wa muhimu sana.

Mpaka sasa Madrid wanaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania ikiwa na pointi sawa na Valencia na Atletico Madrid huku wababe wenzake Bacelona wakiwa nafasi ya saba.

error: Content is protected !!