June 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Real Madrid waingia hofu kutema ubingwa, Barcelona ‘out’

Wachezaji wa Real Madrid

Spread the love

 

IKIWA umesalia mchezo mmoja kukamilika kwa Ligi Kuu Hispania (La Liga), klabu ya Real Madrid ipo shakani kupoteza ubingwa wa Ligi hiyo kutokana na kuwa nyuma kwa pointi mbili dhidi ya kinara Atletico Madrid. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mpaka sasa Ligi hiyo imeshachezwa michezo 37 huku Atletico Madrid wakiwa kileleni kwa pointi 83, wakati Real Madrid wakishika nafasi ya pili kwa pointi 81 na Barcelona kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi 76 ambao wameshatolewa kwenye mbio za ubingwa.

Vinara hao wanahitaji kushinda mchezo wao wa mwisho utakaopigwa siku ya Jumapili dhidi ya Valladolid waliopo kwenye nafasi ya 19, ambao nao wanahitaji pointi tatu ili wasishuke daraja.

Wachezaji wa Atletico Madrid

Kwa upande wa Real Madrid, wanahitaji kushinda mchezo wao wa mwisho ambao watamenyana na Villareal, huku wakiombea mabaya majirani zao Atletico Madrid kupoteza mchezo wao.

Real Madrid kwa sasa ndiyo mabingwa watetezi taji hilo ambalo walitwaa msimu uliopita chini ya kocha wao Zinedin Zidane ambaye ametanabaisha kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu unapomalizika.

error: Content is protected !!