July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

REA kuneemesha vijiji 7,873

Mafundi Umeme wakiwa kazini

Spread the love

SERIKALI kupitia Wakala Nishati Vijijini (REA), imeanza awamu ya tatu ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme vijijini na kutangaza kuanza kupokea maombi ya wazabuni, anaandika Pendo Omary.

Awamu hiyo ya tatu, itajumuisha vijiji 7,873 kutoka wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara na utatekelezwaji utafanyika kwa kuanzia mwaka 2016 hadi 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Boniface Gissima, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA amesema miongoni mwa vijiji hivyo, vijiji 7,697 vitapelekewa umeme wa gridi na vijiji 176 vitapata umeme wa nje ya gridi kutokana na nishati jadidifu.

“Hadi kufikia sasa, jumla ya vijiji 4,395 kati ya vijiji 12,268 ambayo ni sawa na aailimia 36 vimeunganishwa na huduma ya umeme.

“Sh. 7,000 Bilioni zitatumika kusambaza umeme wa gridi ambapo kati ya fedha hizo Sh. 4,000 Bilioni ni kwa ajili ya kufisha umeme kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme katika wilaya na mikoa yote, amesema Gissima.

Amedokeza zaidi kuwa, Sh. 3,000 Bilioni ni kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye maeneo ambayo yameshafikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vitongoji na taasisi bado hazijafikiwa na umeme na gharama halisi zitabainishwa baada ya zabuni kufanyiwa uchambuzi.

“Fedha hizi zitatoka kwenye bajeti ya maendeleo ya serikali kila mwaka; tozo kwenye petroli na mafuta ya taa, tozo ya umeme na michango ya washirika wa maendeleo na mradi huu utatekelezwa na sekta binafsi” ameeleza Gissima.

Aidha, ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla.

error: Content is protected !!