Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko RC Sh’nga awapigania wakulima wa choroko, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

RC Sh’nga awapigania wakulima wa choroko, atoa maagizo

Choroko
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga (RC), Zainab Telack, ameagiza maafisa kilimo mkoani humo, kutoa elimu ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa wakulima wa zao la choroko ili waache tabia ya kuuza mazao mapema. Anaripoti Danson Kaijage, Shinyanga … (endelea).

Amesema, hatua hiyo itaondoa dhana ya kuwanufaisha wanunuzi badala ya wakulima ambao wanatumia nguvu nyingi kuandaa mazao hayo.

Zainab amesema hayo jana Jumatatu tarehe 11 Januari 2021 wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku moja kilichowakutanisha wadau wa zao la choroko mkoani humo ili kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa lengo la kuhakikisha unaleta tija kwa wakulima wa zao hilo na taifa kwa ujumla.

Alisema kutumia mfumo wa stakabadhi gharani, utawezesha wanunuzi wa zao la choroko kujua sehemu sahihi ya kupata zao hilo likiwa katika ubora na kuepuka kuibiwa fedha zao na matepeli.

RC huyo alisema, ni agizo la serikali kuhakikisha mazao ya aina ya kunde yanatumia mfumo stakabadhi gharani kama ilivyo kwa zao la korosho na sasa Shinyanga kwa kuanzia, inaanza na zao la Choroko na baadae itahamishia nguvu kwenye zao la dengu na mpunga lengo likiwa kuahakikisha wakulima wa mazao haya wanapata faida ya jasho lao na kujiletea maendeleo.

“Nataka kuona wakulima mkoani Shinyanga, wakiwa na uwezo wa kusomesha watoto, kujenga nyumba bora na kufaidika na jasho lao.”

“Sio mkulima analima mpunga katika maji mengi lakini mnunuzi ananunua mpunga bado ukiwa shambani na kuvuna gunia sitini kwa kumlagai mkulima kwa kumpatia bodaboda,’’ alisema Zainab.

Pia, mkuu huyo wa mkoa, alimwagiza Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Hilda Simon kukutana na viongozi wa vyama vya msingi na cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) kuweka mikakati ya pamoja ya kutoa elimu kwa wakulima ili wajue faida za kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.

Naye Hilda alisema, changamoto ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani inasababisha kushindwa kuwa na takwimu sahihi za zao hilo, kuendelea kuwepo kwa utoaji vibali holela vilivyokuwa vikitolewa na halmashauri bila kupitia vyama vya Msingi.

Hilda alisema, vibali hivyo vilikuwa vikitolewa kwa wanunuzi wa kati ambao kimsingi ndio wapinzani wa mfumo wa stakabadhi gharani na hivyo kuendelea kumyonya mkulima kwa kununua choroko kwa bei za chini.

Alitaja changamoto ya wakulima kukosa uvumilivu wa kusubili malipo kuwa ni sababu ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa aliwaambia wadau wa kikao hicho kuwa viongozi wa vyama vya msingi mkoani humo ni tatizo kwakuwa hawajui uchungu wa wakulima kwani hawana hata shamba moja kazi yao imekuwa ni kuongea maneno maneno tu nakuwataka wakulima kuchagua viongozi ambao pia wana mashamba ya zao hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!