June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mulongo: Miundombinu Mwanza ni tatizo

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema Jiji la Mwanza limekithiri kuwa na miundombinu mibovu kitendo kinachochangia ukusanyaji mdogo wa mapato na kufikika kwa huduma mbalimbali. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kwa mjibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mwanza unakusanya Sh.  123 bilioni ikiwa ni chini ya lengo lao la ukusanyaji wa Sh. 7.69 trilioni katika kipindi cha mwaka 2014/15.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la simu nchini (TTCL) ambapo alisema miundombinu mibovu katika Jiji hilo inachangia shughuli za maendeleo kukwama pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mulongo amesema kuwa mpangilio mbovu uliopo katika Jiji hilo lililozungukwa na milima na miamba umeonekana kurudisha nyuma ukusanyaji wa mapato pamoja na ufikishaji wa huduma kwa wananchi.

Pia amesema miundombinu hiyo imekuwa ikichangia wananchi kushindwa kuendesha shughuli zao za kila siku ambazo zingesaidia taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020 na kwamba changamoto hiyo imekuwa ni kero kwa ukuaji wa taifa.

“Mwanza (Jiji) miundombinu yake ni shida na ni changamoto sana, hali hii inachangia watu walio wengi kuendesha shughuli zao kwa taabu hivyo ni lazima tatizo hilo lishughulikiwe mapema iwezekanavyo.

“Nyie (wafanyakazi wa TTCL) mmeeleza kwamba mnashindwa kuwafikia wananchi kwa sababu ya miundombinu mibovu, ni kweli hilo halipingiki mwanza miundombinu ni tatizo kubwa,” amesema Mulongo.

Hata hivyo amesema kutokana na hali hiyo aliwahakikisha wakazi wa Mwanza kwamba miundombinu hiyo itashughulikiwa kwa kuishauli mamlaka husika kutengeneza barabara ambazo hazipitiki ili kuingeza tija ya ukuaji wa maendeleo.

Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Johnbosco Kalisa, amesema  katika kipindi cha 2014/15 wamekusanya Sh. 123 milioni na kwamba wakati mwingine ukusanyaji huo hupungua hadi millioni 100 kutokana na watumiaji kuwa wachache.

Amesema licha ya watumiaji wa huduma hiyo kuwa wachache pia miundombinu ya barabara katika Jiji hilo huchangia shirika hilo kukusanyaji mapato kidogo hivyo kuna haja ya kuboresha miundombinu hiyo.

error: Content is protected !!