January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mulongo awatisha wafanyabiashara Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amewaonya Wafanyabiashara na watu wanaotumia uwezo wa mali kuwatishia maisha binadamu wenzao na wakati mwingine kukatisha uhai wao, kuacha mara moja. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa  wakati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, juu ya utekelezaji wa uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura, hali ya usalama mkoani humo na suala la uchuguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Mulongo amesema wafanyabishara walio wengi wamekuwa wakitumia uwezo wa mali zao kuwatishia watu, huku wakijinasibu wapo karibu na Serikali hawataweza kufanywa lolote.

Kauli ya mulongo inakuja ikiwa hivi karibuni kutokea tukio la mfanyabiashara na mmliki wa mabasi ya J4, Juma Mahende, kuwauwa watu wawili kwa risasi, Ali Mohamed mkazi wa Igoma na Cloud Steven, mkazi wa Nyansaka.tumia slaha yake.

Mulongo amesema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiwatishia watu, huku wakishindwa kufahamu nguvu ya dola licha ya kujinasibu kwamba Serikali haiwezi kuwachukulia hatua kwa sababu ya utajiri wao. 

“Wapo Wafanyabiashara wanaotumia uwezo9 wao kutaka kuwanyanyasa wenzao na wanawanyima watu haki zao kwa ubabe, wengi wanajitapa mtaani Serikali haiwezi kuwafanya chochote.

“Hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, kama mkoa tutawashughulikia watu wa aina hiyo, vitendo hivyo haviwezi kuvumiliwa hata siku moja kwa sababu wanafanya mambo hayo kwa dharau,” amesema Mulongo.

Katika hatua hiyo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi pale ambapo kuna kitendo kinachoashiria kuwepo kwa uvunjifu wa amani ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema.

Sanjari na hayo  amesema Mkoa wa Mwanza, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura, ikilinganishwa na mikoa mingine hapa nchini.

Amesema katika Mkoa huo wamefanikiwa kuandikisha watu 144,2391 ambamo wanawake 739, 786 na  Wanaume ni 702, 6005, huku akisema lengo lilikuwa ni kuandikisha watu 1,403, 743 sawa na asilimia 103.

error: Content is protected !!