January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mulongo atuhumiwa ufisadi

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo anatuhumiwa kukwapua Sh. Mil 10 za safari ya kikazi Dubai na kisha kutokomea. Anaandika Moses Mseti … (endelea).

Safari hiyo ilihusu kwenda kujifunza namna bora ya upangaji wa Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela.

Katika ziara hiyo ya mafunzo, kiasi cha Sh. Mil 100 zilitumika kwa ajili ya posho za kujikimu, usafiri wa ndege wa kwenda na kurudi kwa siku 10 za mafunzo hayo Dubai.

Mingoni mwa waliokuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Faisal Issa; Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga; Meya wa manispaa hiyo, Henry Matata na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, John Mpemba. 

Jiji la Mwanza liliwakilishwa na Meya, Stanslaus Mabula; Ofisa Uhusiano, Joseph Mlinzi huku Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Adam Chagulani akienguliwa katika safari hiyo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi walioenda ziara Dubai, wameliambia Mwanahalisi online, Mulongo alichukua kiasi hicho cha fedha kwa madai ya kutangulia lakini hakuonekana Dubai kwa siku zote walizokaa huko.

Mwandishi alipompigia simu zaidi ya mara nne ili kujua ukweli wa tuhuma zake, licha ya simu yake kuita, Mulongo hakupokea.

Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ulioeleza madai hayo, Mulongo alijibu “Issue nini, kama si kwenda au nilienda, yaani tatitizo unachotaka kujua nini.”

Mwandishi aliamua kumpigia simu tena, simu yake tayari ilikuwa imezimwa. Hata hivyo mwandishi alimtumia ujumbe wmingine akisisitiza kupata majibu ya maswali yake lakini Mulongo alijibu ‘No Comments.’ 

Mmoja kati ya wajumbe waliosafiri alilieleza MwanaHALISI online kuwa, “Kila mtu hapa anamjua Mulongo jinsi alivyo mbabe, haiwezekani akachukua fedha alafu asionekane katika ziara hiyo ambayo ilikuwa ni mhimu sana, amekuja kuharibu Mkoa wetu.” 

Hata hivyo inadaiwa kuwa viongozi hao walikwenda kujifunza Dubai kutokana na mji huo kuwa na miundombinu na upangaji mji vizuri, kabla ya kutwa maeneo ya mipaka ya Wilaya ya Magu na Misungwi kwa ajili ya kujenga vitega uchumi.

Hivi karibuni, Mulongo aliingia katika mgogoro na baadhi ya viongozi wa Mkoa Mwanza hususan Mkurugenzi, Halifa Hida kwamba, anakwamisha juhudi za maendeleo na upangaji wa jiji hilo na kusababisha mvutano mpaka sasa.

error: Content is protected !!