July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mulongo atoa siku 14 madai CWT

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amempa wiki mbili Mkurugenzi wa Halmashauli ya Wilaya ya Sengerema, Julias Chalya kuhakikisha anawalipa Walimu 778 madai yao. Anaandika Moses Mseti … (endelea).

Pia amemtaka mkurugenzi kuhakikisha anawabaini watu wanaosababisha madai ya walimu hao yachelewe kupatiwa ufumbuzi ili waweze kuchukuliwa hatua na kuwa fundisho kwa watu wengine.

Chama cha Walimu Wilaya ya sengerema (CWT) mkoani Mwanza kinaidai serikali zaidi ya shilingi 700 milioni ikiwa ni miongoni mwa fedha za mishahara, fedha za likizo na kupandishwa cheo.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauli hiyo, juu ya mgogoro uliyopo baina ya walimu na serikali pamoja na kujengwa nyumba katika bomba kuu la maji wilayani humo.

Mulongo amesema kuwa mgogoro uliyopo katika halmashauli hiyo unatokana na baadhi ya watumishi kushindwa kufanya kazi zao ipasavyo kitendo kinachosababisha walimu kuendelea kuida serikali kwa kipindi kirefu sasa.

Amesema watumishi wazembe na mizigo katika halmashauli hiyo wamekuwa ni chanzo cha migogo, na kwamba watu watumishi wa aina hiyo hawapashi kuendelea kuitumikia jamii na badala yake wanapaswa kutafuta kazi nyingine ya kufanya.

“Hivi Mkurugenzi (Julias Chalya) tangu mwezi wa sita (juni) mwaka huu mpaka leo mnashindwa kushughulikia matatizo ya walimu, sasa kuanzia leo (juzi) nawapa wiki mbili kuwalipa madai yao yote,” amesema Mulongo.

Mkurugenzi wa halmashauli hiyo, Julias Chalya, amekiri wazi walimu hao kuidai serikali na kwamba mipango ya kuwalipa walimu hao ilikuwa imeanza na ilikuwa katika hatua za mwisho za kuwalipa stahiki zao.

Chalya amesema kuwa walimu 778 katika wilaya hiyo wanaidai serikali, mishahara, fedha za likizo na madeni yasiyoingiliana na mishahara huku walimu 234 wenye madai ya kupandishwa madaraja kulingana na muda wao kazini bila kupandishwa madaraja.

Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Sengerema (CWT), Ruhumbika Francis, amesema CWT wilayani humo wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu lakini mkurugenzi wa halmashauli hiyo amekuwa akishindwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

error: Content is protected !!