Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Mtaka awafunda Ma-DC ‘epukeni balehe ya madaraka’
Habari za Siasa

RC Mtaka awafunda Ma-DC ‘epukeni balehe ya madaraka’

Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma (RC), Antony Mtaka amewataka wakuu wa wilaya (DC), kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuachana na tabia ya ulimbukeni ya madaraka ‘balehe ya madaraka.’ Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Mtaka ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 22 Juni 2021, mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi na wa Kongwa, Remidius Emmanuel.

Mtaka amesema, wakuu hao wa wilaya wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo ya kazi na kujiepusha na kutumia mabavu kwa watu wanaowaongoza.

“Nataka niwafunde nyie wakuu wa wilaya ambao mmepata madaraka, jambo la msingi jiepushe kuwa watu wa balehe ya madaraka katika maeneo yenu ya kazi.”

“Msiwe washamba wa madaraka kwa kutumia madaraka yenu vibaya, kwa kutumia mabavu na kudhani kila jambo mnaweza kulifanya bila kuwashirikisha watu wengine kwenye ofisi yako,” amesema Mtaka

“Watu wengi wanapokuwa madarakani wanakuwa washamba au limbukeni na bora mfanyabiashara anaweza kupata fedha akawa limbukeni lakini mtu ambaye akipata cheo anaweza kuwa limbukeni mara tatu, sasa nasema jiepusheni na balehe ya madaraka mtaharibikiwa,” amesema

Mtaka amesema “najua kuwa mnapokuwa kazini mtapata marafiki wa majina na marafiki wa vyeo, marafiki wa majina watawaambia ukweli juu ya utendaji wa kazi na wakati mwingine hamtawapenda lakini hao ndio watakao wasaidia katika utendaji wa kazi.”

Mkuu huyo wa mkoa ameendelea kuwaasa akisema “lakini wapo marafiki wa vyeo ambao kila saa ni kuwapamba na kukusifia kwa kila jambo hata ukiwa umeharibu utasifiwa ili mradi tu wakupambe na kukuambia ndiyo mzee huku ukiwa unaharibu kazi ambayo umepewa kulifanya.”

Amewaonya na kuwataka kuwa watumishi wa watu badala ya kuwa watawala kwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwaonea na kuwatesa watu wengine.

“Unapokuwa kiongozi kubali kusikiliza maoni na ushauri wa watu wengine ndani ya ofisi na usipende kutumia madaraka kuonekana kuwa wewe ni bora zaidi ya mwingine,” amesema

“Ili kuweza kufanya jambo la msingi na lenye tija ni lazima kufanya kazi kwa kushirikiana ni wazi kuwa mtakwama na mtakuwa mmeskia aibu kwa mtu aliyewateua” amesema Mtaka.

Katika hatua nyingine, Mtaka amewataka wakuu hao wa wilaya katika wilaya zote za Dodoma kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele badala ya kwenda kwenye wilaya na kuanza kuzua migogoro na ugomvi kati ya wao na jamii inayowazunguka.

“Mimi sihitaji kusikia wilaya ina migogoro na wananchi na sipo kwa ajili ya kusuruhisha migogoro, mimi nataka kusikia maendeleo yanayofanyika na mkumbuke kuwa wakuu wa wilaya siyo wasaidizi wa mkuu wa mkoa bali ni wasaidizi wa Rais katika wilaya husika.”

“Kwa maana hiyo nataka kuwaambia kuwa kila mmoja afanye kazi kulingana na uwezo wake wa kufanya kazi” amesema Mtaka.

Kwa upande wake, Mwema ameapishwa huku akihaidi kutoa uhirikiano wa kimaendeleo pamoja na kuwa karibu na viongozi pamoja na wananchi na “kuhakikisha natekeleza maagizo ya Rais kwa manufaa ya wananchi wote.”

Naye Mkadachi amesema yeye katika utumishi wake, atajipambanua na baadhi ya wale wanaoongoza kitawala na badala ya kuongoza kiutawala.

“Mimi nitakuwa tofauti katika utumishi wangu, kwani sikakuwa mtawala bali nitakuwa kiongozi katika utumishi wangu. Pia, nitakuwa ni mnyenyekevu na kushirikiana na kila mwananchi na viongozi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!