Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Mtaka ataka walimu kutawanya Dodoma, kila mwanafunzi apate mti
Habari Mchanganyiko

RC Mtaka ataka walimu kutawanya Dodoma, kila mwanafunzi apate mti

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa (RC) wa Dodoma nchini Tanzania, Antony Mtaka ameuagiza uongozi wa ofisi ya mkurugenzi wa jiji na afisa elimu kuhakikisa wanawasambaza walimu wa sekondari katika shule zenye uhaba badala ya kuacha walimu kurundikana shule moja. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mtaka amesema zipo shule za sekondari ndani ya Jiji la Dodoma ambazo zina walimu wengi na zipo shule za sekondari ambazo zipo pembezoni mwa jiji hilo zina walimu wachache.

Kutoakana na hali hiyo, ofisi ya afisa elimu na ofisi ya mkurugenzi wa jiji waone namna ya kuweza kuwasambaza walimu waliokuwa wengi katika shule za mijini na kuwapeleka katika shule za pembezoni ambazo zina uhaba wa shule.

RC Mtaka ametoa maelezo hayo leo Jumatano tarehe 22 Desemba 2022, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondori kwa fedha za mkopo wa masharti nafuu unaotokana na mapambano dhidi ya Uviko -19.

Amesema Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa ambayo imefanikiwa kufanya ujenzi wa vyumba bora vya madarasa ambayo yana ubora wa kiwango cha juu.

Moja ya misitu iliyopo nchini Tanzania

“Dodoma tumeweza kujenga madarasa yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha lakini napenda kutoa maagizo katika ofisi ya mkurugenzi na afisa elimu kukutana mkaona ni namna gani ya kufanya utaratibu wa kupunguza walimu waliozidi katika baadhi ya shule na kuwapeleka katika shule ambazo zina uhaba wa walimu,” amesema

“Na jambo hili liwekwe wazi kwa walimu kuwa ni kwa nia njema ili kuifanya elimu ya wanafunzi wa Jiji la Dodoma kuwa bora zaidi na ilingane na viwango vya ubora wa madarasa” amesema Mtaka.

Aidha, ameto maelekezo kwa ofisi ya mkurugenzi wa jiji la Dodoma na ofisi ya afisa elimu wa Jiji kutoa taarifa kwa wakuu wote wa shule kuwa pindi shule zitakapofunguliwa tarehe 17 Januari 2021 kila mwanafunzi katika shule zote za sekondari na msingi za serikali na binafsi kila mwanafunzi awajibike kupanda mti na kuutunza.

“Kila shule ya msingi na sekondari, ya serikali au binafsi nilazima kila mwanafunzi wakati wa kufungua shule apande mti na kuhakikisha anautunza na upandaji miti huo uwe na miti ya kivuli na matunda.

“Tukiwa na miti mingi ya kutosha ya matunda na kivuli tutakuwa tumejiongezea sana thamani ya utunzaji wa mazingira pamoja na kuondokana na udumavu kwani watoto wataweza kula matunda,” amesema Mtaka.

Katika maagizo mengine muhimu aliyoyaagiza Mtaka ni kuhakikisha watoto wote wenye sifa ya kwenda shule iwe sekondari au msingi wanaenda shule bila kuwekewa na vikwazo vyovyote.

“Itakuwa ni aibu kubwa kuwa na majengo mazuri na ya kisasa ambayo yanajitosheleza lakini watoto hawahendi shule, hatutaki kuona watoto wanakosa masokoni, mitaani pamoja na kuchunga mifugo au watoto kuwa sehemu ya kuitunza familia” amesisitiza Mtaka.

1 Comment

  • Maelekezo ya RC kuhusu wanafunzi kupanda miti ni mwafaka kwa kampeni ya Dodoma ya Kijani. Aidha, namuomba atoe maelekezo mengine kwa viongozi wa Serikali za mitaa kusimamia suala la upandaji miti kwa wakazi wa mitaa yao. Mkoa uweke mfumo wa ufuatiliaji wa karibu kupitia serikali za mitaa kuhakikisha wananchi wote wa Dodoma tunapanda walau miti mitano kwa mwaka na kuitunza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!