Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko RC Mtaka aipongeza NMB, vifaa vya mamilioni vyatolewa Dodoma
Habari Mchanganyiko

RC Mtaka aipongeza NMB, vifaa vya mamilioni vyatolewa Dodoma

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma (RC) Anthony Mtaka ameitaka Benki ya NMB kutochoka au kurudi nyuma katika kuisaidia jamii nzima ya Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema hayo leo Jumatatu, tarehe 4 Oktoba 2021, aliposhiriki uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa weteja na ahadi hiyo ipo kwenye Hati ya Kiapo cha benki hiyo ambazo kitaifa imefanyikia jijini Dodoma.

RC Mtaka amesema hayo baada ya kuelezwa na Afisa Mtendaji Kuu wa NMB, Ruth Zaipuna kusema, maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na kutoa misaada mbambali mkoani huo yenye thamani ya Sh.40 milioni ya kiwemo madawati na vifaa vya hospitali.

Mkuu huyo wa mkoa amesema, benki hiyo imekuwa ikisaidia maeneo mbalimbali kwenye jamii ikiwemo sekta za afya, maji, afya na elimu na kuitaka “kutochoka na ukarimu wanu ambao hata viongozi wengine wanasema umekuwa chachu kubwa ya kuyabadilisha maisha si tu ya wakazi wa Dodoma bali pia Tanzania nzima.”

“Suluhishi zenu bunifu za kifedha na uwekezaji mkubwa mnaoendelea kuufanya ni vitu vinavyoifanya NMB kuwa benki kubwa na kiongozi wa maendeleo nchjini,” aliongeza RC Mtaka alisema.

Katika maelezo yake, Afisa Mtendaji Kuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema, Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Mteja ni nyenzo muhimu katika kuweka uhusiano mzuri na wateja wa benki hiyo ili waendelee kuiamini na iweze kuendeleza ushindani wenye tija sokoni.

Amesema, mkataba huo wa hiari pia unaiwezesha NMB kuweka maazimio ya uhusiano wa kibiashara wenye afya na wateja wake.

“Leo tunaungana na dunia nzima kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, inayoadhimishwa kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba,” amesema Zaipuna

“Kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu ni ‘Nguvu ya Huduma’ na ili NMB iendelee kuongoza kwenye utoaji huduma kwa wateja, maadhimisho haya tunayatumia kuzindua Hati ya Kiapo cha Huduma kwa Mteja kuonyesha kwa vitendo nguvu ya huduma kwa wateja wetu,” kiongozi huyo alifafanua.

Zaipuna amesema kimsingi hati hiyo ina ahadi tano za benki kwa mteja ambazo ni kupatikana kwake kwa haraka, usikivu, uhakika na kuaminika, usalama wa taarifa za mteja pamoja na weledi na nidhamu.

Akiwapongeza wateja kwa kuiunga mkono benki hiyo na kuchangia mafanikio yake, Zaipuna alifafanua kuwa ahadi hizo ni maazimio yatakayolinda haki ya mteja na pia yenye kudhamiria kudumisha uhusiano wao mzuri.

“Mbali na wateja, naomba pia niwashukuru wafanyakazi wenzangu wa Benki ya NMB kwa kazi kubwa wanayofanya, benki hii imekuwa ikiongoza kwa kila kitu sababu ya utendaji mzuri na uaminifu wao, na ndiyo nguzo tunayosimamia,” alisisitiza.

Katika uzinduzi huo, benki hiyo imewatunuku vyeti maalum wateja na wafanyakazi wake ambao ndiyo wachagiaji wakubwa wa mafanikio yake. Kupitia, hati hiyo ya kiapo, watumishi wa NMB wanajua nini kinategemewa kutoka kwa wakati wa kutoa huduma na wateja nao wanapata haki ya kujua nini watarajie kutok benki hiyo.

Zaipuna amesema kimsingi hati hiyo ina ahadi tano za benki kwa mteja ambazo ni kupatikana kwake kwa haraka, usikivu, uhakika na kuaminika, usalama wa taarifa za mteja pamoja na weledi na nidhamu.

Akiwapongeza wateja kwa kuiunga mkono benki hiyo na kuchangia mafanikio yake, Zaipuna alifafanua kuwa ahadi hizo ni maazimio yatakayolinda haki ya mteja na pia yenye kudhamiria kudumisha uhusiano wao mzuri.

“Mbali na wateja, naomba pia niwashukuru wafanyakazi wenzangu wa Benki ya NMB kwa kazi kubwa wanayofanya, benki hii imekuwa ikiongoza kwa kila kitu sababu ya utendaji mzuri na uaminifu wao, na ndiyo nguzo tunayosimamia,” alisisitiza.

Misaada ambayo NMB imeitoa mkoani humo ni pamoja na vifaa vya hospitali kwa ajili ya Hospitali Wilaya ya Bahi na Zahanati ya Chimedeli.

Pia vimo viti 200 na meza 200 kwa ajili ya shule za sekodari Nondwa, Msisi Juu, Sechelela na Ibihwa pamoja na madawati 50 kwa ajili ya Shule ya Msingi Chiguluka na mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Bahi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wake wa wilaya na wabunge wa Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!