May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC mstaafu Kigoma afariki dunia

Brigedia Jenerali, Emmanuel Maganga

Spread the love

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Kigoma (RC), Brigedia Jenerali, Emmanuel Maganga, amefariki dunia jana Alhamisi saa 3 usiku tarehe 21 Januari 2021, katika Hospitali ya Milambo, Mkoa wa Tabora alipofikishwa kwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Philemon Sengati amesema, “amefariki kwenye hospitali ya Milambo, hakuwa amelazwa, alikuja akitokea kwenye ujenzi kwenye eneo lake, alikuwa na presha na kisukari na presha ilikuwa imepanda.”

Dk. Sengati amesema, leo Ijumaa tarehe 22 Januari 2021, taratibu za mazishi zitaanza.

error: Content is protected !!