Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia
Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the love

ALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na Arusha kwa nyakati tofauti, Isdory Shirima amefariki dunia leo tarehe 31 Machi 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, CCM kimepokea kwa masikitiko na huzuni taarifa ya kifo cha mkuu huyo wa mkoa mstaafu.

Mjema pia amemtaja Shirima kuwa kwa nyakati tofauti aliwahi kushika dhamana mbalimbali ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na Katibu Msaidizi Mkuu (CCM) – Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga.

Amesema CCM kitamkumbuka Shirima alivyokuwa mwanachama, mtumishi na Kiongozi mwaminifu, aliyetumia uwezo wake kwa maslahi mapana ya CCM na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi kwa ujumla.

“CCM chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa Chama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kinatoa salaam za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa CCM na wote walioguswa na msiba huu. Mungu ailaze roho ya marehemu mąhali pema peponi, Amina,” amesema mjema katika taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!