December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mbeya sasa kuchapa viboko wasiofunga ndoa

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Spread the love

ALBERT Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametangaza kuwachapa bakora wanaume na wanawake wasiofunga ndoa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Chalamila ametangaza kampeni hiyo kufuatia mijadala iliyoibuka mitandaoni hivi karibuni, juu ya changamoto ya wanawake wengi kutoolewa, ambapo baadhi ya wananchi wakinyooshea vidole wanaume kwamba wamekuwa wagumu kuoa.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza, mwanamke atakayekutwa hajaolewa, na mwanaume atakayekutwa hajaoa, atatatindwa bakora ili akatafute mume au mke.

“Maana siku hizi tunaanza kutumia viboko katika kila jambo, hata tukikuta umekaa pale nyumbani huolewi ni bakora tu, nenda katafute mume.

“Tunakuona umekee pale nyumbani huoi ni bakora tu nenda katatufute mke. Kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe kwa hiyo viboko vinasaidia,” amesema Chalamila.

error: Content is protected !!