May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar azuia wasiovaa barakoa kupanda daladala, mwendokasi

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amewataka madereva na makodakta wa vyombo vya usafiri jijini kutowabeba abiria wasiovaa barakoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, amelitaka Jeshi la Polisi, wakuu wa wilaya (DC)na Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri Ardhini (Latra), kusimamia mwongozo wa wizara ya afya, kwenye sekta ya usafirishaji.

RC Makalla ametoa maagizo hay oleo Jumatatu, tarehe 2 Agosti 2021, katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha mkoa ambacho yeye ni mwenyekiti.

Lengo la kikao hicho, kilikuwa kinapitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo uliotolewa na wizara ya afya juu ya kujikinga na corona na kusisitiza vyombo vya usafiri kubeba abiria kulinagana na idadi ya viti ‘level seat.’

Amesema kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya maeneo hivyo polisi, wakuu wa wilaya na Latra wanapaswa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa wizara ya Afya.

Kutokana na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, Makalla ameruhusu daladala kubeba wanafunzi watano watakaosimama lakini kwa kigezo cha wanafunzi hao kuwa wamevaa barakoa.

Aidha, Makalla ameendelea kusisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyokuwa na lazima na Kama ikitokea Kuna ulazima taratibu zote za kujikinga zizingatiwe.

Kuhusu suala la chanjo, amefurahi kuona wananchi wamekuwa na mapokeo makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa mujibu wa mganga mkuu wa mkoa huo hadi kufikia jana Jumaoili, tayari wananchi 10,000 wamefanya ‘booking’ na wanahofia chanjo zitawahi kumalizika.

error: Content is protected !!