June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar ajitetea, Mahakama yapiga ‘stop’ bomoabomoa

Spread the love

WAKATI mahakama kuu ikisimamisha zoezi la bomoa bomoa, Mkuu wa Mkoa  Dar eS Salaam, Said MeckSadick amejiteteana kukanusha taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa kisiasa hususani wenyekiti wa mitaa na baadhi ya wakazi  wanaoishi maeneo hatarishi ya mabondeni juu ya serikali kuvunja nyumba, ikizingatia kutotoa maeneo mbadala ya kujenga makazi mapya ya kudumu. Anaandika Aisha  Amran …. (endelea).

Mecksadick amesema mwaka 2011 yalipotokea mafuriko serikali  iliwapatia viwanja wakazi waliokuwa na nyumba katika maeneo  hatarishi  ya  mabondeni kwa Wilaya zote  tatu za Mkoa Dar es Salaam katika eneo la Mabwepande wilaya Kinondoni.

Kwa mujibu mkuu wa mkoa jumla ya viwanja 1007 viligawiwa kwa wakazi hao wa mabondeni na viwanja vitatu havigukawiwa kwa sababu viliangukia maeneo yasiyofaa kwa makazi.

Aidha sambamba na kupatiwa viwanja wakazi hao walipatiwa misaada ya kibinadamu pamoja na vifaa  vya kiujenzi ikiwemo mifuko ya saruji 100 mabati na mbao kila kaya na kuwawekea huduma muhimu  za kijamii.

Amesema wakazi hao wamediriki kuuza viwanja vyao kwa bei ya chini na kurudi maeneo waliokuwa  wakiishi awali na wengine kuuza na kupangisha nyumba zao walizojenga mabondeni licha ya Serikali  kuwataka waondoke katika maeneo hayo hatarishi.

Vile vile amesema Serikali kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini imeanza na inaendelea na zoezi la bomoa bomoa kwa ajili ya kuwaondoa wakazi wote wanaoishi maeneo hatarishi  na  wale waliovamia maeneo yasiyostahili kujengwa.

Pia amesema zoezi hili la bomoa bomoa litafanyika nchi nzima ambapo kwa sasa limeanzia Mkoa Dar es Salaam na  wakazi waliojenga katika maeneo  hatarishi wabomoe wenyewe na kuondosha baadhi ya  vifaa vya ujenzi ambavyo vitawasaidia kwenda kuendeleza makazi mapya katika viwanja walivyopewa na serikali.

Amewataka wananchi kuacha kuendelea kulalamika wakati wanafahamu kuwa wamevunja sheria licha ya serikali kuwataka kuondoka kabla hawajapata madhara ikiwemo kuvunjiwa nyumba zao.

Wakati Mkuu wa Mkoa akitoa kauli hiyo, Mahakama ya Kuu ya Ardhi imetoa amri ya kusitisha zoezi hilo la kubomoa hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa mahakamani hapo itakaposikilizwa.

Ombi hilo lilitokana na malalamiko ya wakazi wengi walioiomba mahakama izuie bomoabomoa hiyo kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki zao ambapo wengi wa walalamikaji hao walidai kufidiwa kabla ya kuondoka.

Hata hivyo uamuzi huo wa mahakama umewagusa walalamikaji 674 tu ambao wametajwa kwenye malalamiko huku zoezi la bomoabomoa likiendelea kama kawaida kwa nyumba zingine ambazo hazihusiki na kesi hiyo.

error: Content is protected !!