July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar ahimiza sensa ya viwanda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq

Spread the love

SAID Meck Sadiq, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam amevitaka viwanda vya Tanzania Bara kukamilisha taarifa za sensa kabla ya 31 Agosti mwaka huu, kabla ya hatua kali kuchukuliwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea)

Aidha, ukusanyaji wa taarifa za sensa ya viwanda nchini ulianza mnamo mwaka 2003, ambapo mwaka huu ulianza Machi 9 na ulitarajiwa kumalizika  Juni 8 nwaka huu.

Ambamo, kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu jumla ya viwanda Dar es Salaam vipo 1840, na hadi sasa kuna viwanda vipatavyo 366 havijapeleka taarifa zake.

Sadiq amesema, wamelazimika kuongeza muda wa mwezi mmoja kutokana kwamba kuna baadhi ya viwanda havikutoa ushirikiano pindi walipotakiwa kukamilisha dodoso  ili kupelekwa katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Ameeleza kuwa, wamiliki wengi wa viwanda wamekuwa wakidharau madodoso hayo pindi wanapotembelewa na wahusika, wakizani kuwa wanapotezewa muda kumbe ni kwa faida yao ili kuweza kukamilisha taarifa zao za viwanda.

Akizungumzia wahusika wa ukusanyaji wa dodoso hayo kuwa, “taarifa zote zinazohusu viwanda kwa nchi nzima, hukusanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na biashara, ambamo huweza kutambua kama kiwanda kipo hai au hakipo tena ”

Amezungumzia lengo na faida ya sense hiyo kuwa, takwimu sahihi za viwanda husaidia kupata viashiria sahihi vya uchumi pamoja na kupata taarifa muhimu kama, orodha ya viwanda kimkoa, anuani na viwanda vilipo, aina ua umiliki.

Lengo lingine, utaifa wa wamiliki, mwaka ambao viwanda hivyo vimeanza uzalishaji, shughuli kuu ya viwanda, wafanyakazi, mapato yatokanayo na kiwanda, pamoja na gharama za uzalishaji.

Lingine, ni kuweza kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika sekta ya viwanda ili kuwezesha serikali kuboresha sera na program za kukuza ajira , kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama, malengo ya millennia na dira ya maendeleo ya Tanzania.

“Kuhusu suala la kujua mmiliki na shughuli za viwanda vinatusaidia sana kujua watu wanaomiliki hivyo viwanda je ni wazawa au wahamiaji? Kwaiyo watanzania wasipuuzie hili kwani linafaidi sana kwao na sisi kuangalia jinsi gani ya kuwasaidia kuendelea na biashara zao”. Amesema Sadiqi.

Amesema, kutoa faarisa na kujaza madodoso ni jukumu la kila mmiliki waviwanda, na anapaswa kutoa taarifa zilizosahihi ili kusaidia kupanga mipango mikakati ya maendeleo ya viwanda.

“Nitoe wito kwa wamiliki wote wa viwanda kufuata maelekezo ya serikali l;I kuepusha matatizo yasiyo ya lazma.Kama ilivyo kwa sheria zetu mmiliki wa kiwanda asipo jaza madodoso kwa muda muafa adhabu yake ni jela kwa miezi 6 au hata kiwanda kufungwa”. Amesema Sadiki.

error: Content is protected !!