May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Chalamila: Nimezungumza na Rais Magufuli

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Albert Chalamika

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Mbeya (RC), Albert Chalamika amesema, Rais wa Tanzania, John Magufuli yuko salama na anaendelea na majukumu yake kama kawaida. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Leo Ijumaa tarehe 11 Machi 2021, RC Chalamila amezungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali mkoani huko inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano, huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo.

“Leo asubuhi nimempigia simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumshukuru kwa fedha alizotupa za kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kweli amenijibu kwa furaha na faraja kubwa mno,” amesema RC Chalamila.

Rais John Magufuli

Katika kusisitiza hilo, Chalamila amesema “hao wanaozungumza rais yuko kwenye matibabu labda wao wako kwenye matibabu. Kwa kweli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, he is very strong (yupo imara) na anaendelea kufanya kazi zake vizuri sana.”

RC Chalamila ametoa kauli hiyo, baada ya uwepo wa taarifa mbalimbali mitandaoni kwamba, Rais Magufuli yupo nje ya Tanzania kwa matibabu.

error: Content is protected !!