Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Chalamila atibua nchi, ajitetea
Habari za SiasaTangulizi

RC Chalamila atibua nchi, ajitetea

Spread the love

KITENDO cha Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuingilia majukumu ya walimu wa Shule ya Sekondari Kiwanja, Chunya kwa kuchapa viboko vitatu kila mwanafunzi, kimetibua wengi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Chalamila aliwachapa viboko wanafunzi 14 jana tarehe 3 Oktoba 2019, kwa tuhuma za kuhusika katika kuchoma moto mabweni mawili ya shule hiyo tarehe 1 Oktoba 2019, kwa madai ya kupanga tukio hilo kupitia mawasiliano ya simu zao.

Video ya tukio hilo, ilisambaa kwa kiwango kikubwa jana na kuibua mjadala. Makundi mbalimbali yanapinga hatua ya Chalamila kuingilia majukumu ya kuadhibu wanafunzi hao licha ya kuwepo kwa taratibu za kisheria shuleni hapo.

Fatma Karume, Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter “Huu ni uvunjifu wa sheria.

“RC haruhusiwi kuwatandika wanafunzi. Huu ni ukatili na ni kosa la jinai,” ameongeza “Hakuna mantiki hapa. RC sio bosi wa Mwalimu Mkuu. RC ni bosi wa wasafishaji mitaa mbona hawaendi kusafisha mitaa kila asubuhi ili wasafishaji walale tu?”.

Dickson Matata, wakili wa kujitegemea akizungumza na MwanaHALISI Online amesema, Sheria ya Elimu Sura ya 353 ya mwaka 2002, Kifungu cha 61(1) (v) kinampa mamlaka Waziri wa Elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakayokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo.

“Waraka wa elimu namba 24 ya Mwaka 2002 imeeeleza anayestahili kutoa adhabu ni mwalimu Mkuu au mwalimu yoyote atakayechaguliwa na Mwalimu Mkuu.

“Kutokana na sheria tulizonazo, hakuna sehemu iliyomtaja Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya kuhusika kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi… kwa mujibu wa sheria hakuna sehemu yoyote inayonesha Mkuu wa Mkoa anahaki ya kufanya alichofanya” amesema Wakili Matata.

Mwanaharakati wa elimu pia mwandishi wa vitabu, Richard Mabala kwenye ukurasa wake wa twitter amehoji “Alichapa viboko vingapi? alifuata sheria ya elimu kweli?”

Mwanasheria Jebra Kambole ameandika “Huyu Mkuu wa Mkoa kuna siku ataenda kituoni akachukue bunduki ili kukamata wezi maana ataona wezi wanasumbua polisi kama wanafunzi wanavyosumbua walimu!!! Unawachapa wewe ndo mwalimu wa shule?”

Mdau mwingine wa elimu Tito Magoti ameeleza, kuwa si jambo lenye kukubalika kwa mwanafunzi kumiliki  simu hasa shule ambayo imeeleza wazi kwamba, kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu.

Kwenye ukurasa wake wa twitter amehoji, Chalamila amepata wapi mamlaka ya kuchapa wanafunzi viboko wakati shule ina walimu na taratibu zake katika kuadhibu?

“Si ruhusa wanafunzi kumiliki simu shuleni lakini RC Mbeya ametoa adabu kwa sheria ipi? Mihemko tu, amevunja sheria za nchi, amedhalilisha watoto mbele ya vyombo vya habari. Amepiga na kujeruhi na amejichukulia sheria mkononi.”

Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) katika ukurasa wake wa twitter ameandika “nakemea kitendo hiki cha kikatili. Adhabu ya viboko ni kikatili na inayodhalilisha utu.

“Pia nakemea kitendo cha Mkuu wa Mkoa kutumia madaraka yake vibaya kwa kutenda kinyume cha taratibu za adhabu kwa wanafunzi. Mwenye mamlaka ya kumwadhibu mwanafunzi ni mwalimu mkuu.”

Hata hivyo, Chalamila amesema kitendo chake kimezua mjadala kwenye mitandao hasa hoja kwamba, akustahili kuwachapa viboko wanafunzi hao.

Katika hoja hiyo, akiwa mbele ya wanafunzi wa shule hiyo leo tarehe 4 Oktoba 2019, amesema kama mkuu wa shule anaruhusiwa kuchapa viboko, yeye anaruhusiwa kuchapa zaidi kwa kuwa ndio bosi wa mkuu wa shule.

“Mtakumbuka jana nilikuwepo hapa nilipiga vijana viboko, wengine wamenijadili sana kwenye mitandao kwamba Mkuu wa Mkoa anatoa wapi mamlaka haya?

“Mkuu wa Shule bosi wake ni mkuu wa mkoa, kama yeye anaruhusiwa kuwachapa basi mimi natakiwa niwacharaze sana” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!