May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Chalamila aitisha maombi kumwombea Dk. Magufuli

Albert Chalamila, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Spread the love

 

MKUU huyo wa mkoa wa Mbeya amesema, maombi hayo yatafanyika kesho Ijumaa tarehe 19 Machi 2021, katika Viwanja vya Sokoine jijini Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Chalamila amesema, ibada hiyo maalumu itahudhuriwa na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, viongozi wa kimila na taasisi za umma, wanasiasa pamoja na wananchi wa mkoa huo.

“Siku ya kesho tarehe 19 Machi 2021, Serikali ya Mkoa wa Mbeya imeandaa ibada maalumu, itajumuisha viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, machifu , viongozi waandamizi wa mashirika ya umma,”amesema Chalamila.

Chalamila amesema “maombi maalumu yatafanyika katika uwanja wa Sokoine, kumuombea Rais wa Tanzania kupata mapumziko ya milele na pumziko lenye heri.”

Mbali na kuiombea roho ya Marehemu Rais Magufuli ipumzike kwa amani, pia maombi hayo yatalenga kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha msiba mzito.

“Pia, yatakuwa maombi ya kuombea Taifa ili Mungu aendelee kutulinda ili sisi Watanzania tusivurugane katika kipindi chote cha maombolezo,” amesema Chalamila.

Akitangaza taarifa ya kifo hicho, Mama Samia alisema Rais Magufuli amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya kupata tatizo la maradhi ya mfumo wa umeme wa moyo.

Kabla ya umauti kumfika, Hayati Rais Magufuli aliiongoza Tanzania kwa muda wa miaka mitano na miezi minne, kuanzia tarehe 5 Novemba 2015 hadi 17 Machi 2021.

error: Content is protected !!