August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC azomewa mbele ya JPM

Spread the love

JOHN Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi, mbele ya Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.

Mongella alikumbana na kasheshe hiyo wakati akitoa taarifa fupi ya hali ya usalama na shughuli za maendeleo Mkoa wa Mwanza.

Akiendelea kusoma ghafla wananchi hao walianza kumzomea, hatua ya kuzomea ilianza pale Mongella alipodai kwambwa, hakuna njaa katika mkoa huo.

Mongella amedai kuwa, katika mkoa huo wa Mwanza, wamefanikiwa kuvuna chakula kingi na hakuna tatizo la njaa, kitendo ambacho kilipingwa na wananchi hao ambao walisikika wakidai, “acha uongo’ tuna njaa, hakuna chakula.”

Licha ya zomea zomea hiyo, Mongella aliendelea kueleza kuwa, katika mkoa wake chakula kilichotarajiwa kuvunwa ni tani nane lakini wamefanikiwa kuvuna zaidi ya tani saba sawa na asilimia 93 ya lengo.

“Mpunga kwenye mkoa huu umevunwa mwingi na tumepiga marufuku kuuzwa chakula  nje ya mkoa huu,  huku akidai kwamba kutokana na mavuno hayo, mkoa huo hautakumbwa na njaa,” amesema Mongella.

 

error: Content is protected !!